Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | KUTAF S I R I B I B L I A : MB I NU YA HATUA TATU / 129

wale wasioamini. Kila eneo na hatua ya huduma inahusiana moja kwa moja na umahiri wako wa Neno la Mungu, na utayari wako wa kuruhusu Neno hilo kukutawala! Chukua muda wa kutafakari juu ya viwango vya huduma yako ya sasa nyumbani, kazini, kanisani na katikati ya jamii, na umwombe Roho Mtakatifu akuonyeshe namna ambavyo tafsiri na matumizi yako ya Neno yanaweza kuongeza na kukuza kwa kiwango fulani maisha na ushuhuda wako. Mwombe Bwana akufunulie maeneo fulani ya maisha na huduma yako ambayo yanahitaji nguvu za Neno lake ziwe halisi zaidi na zifanyike kipaumbele chako muhimu zaidi, na uwe tayari kubadilisha mtazamo au tabia yako katika hali yoyote ile ambayo Roho atakufunulia. We Apply theWord of God in Community with Each Other Newbigin anasema kuna njia moja tu ambayo watu wa Mungu wanaweza kuifanya Injili iaminike: “jibu pekee, hemenetiki pekee ya Injili, ni kusanyiko la wanaume na wanawake wanaoiamini na kuiishi . . . wana uwezo wa kutimiza kusudi lao kwa vile tu wamekita mizizi na kurudi katika ushirika wao kama jamii ya waamini.” Hizi eklesia [kanisa, kusanyiko] za watu halisi, katika maeneo halisi, wanaoshughulika na masuala halisi, na wenye ufahamu juu uhalisia wa maisha ya mwanadamu, kama Calvin alivyosema, ni udhihirisho “halisi”wa Kristo duniani kama ilivyo jumuiya ya Mungu mbinguni. Mungu ametupa ahadi za uhakika na za kweli kuhusu nguvu ya maombi ya kutubadilisha, kututia nguvu, na kutupatia mahitaji yetu na maelekezo kutoka kwa Bwana. Kama tulivyoona katika somo hili, haiwezekani kulielewa na kuliishi Neno la Mungu pasipo maisha yenye bidii katika maombi, tena aina ile ya maombi ambayo kwa bidii kubwa na toba tunamwomba Mungu atupatie hekima inayohitajika ili kulijua na kuliishi Neno lake. Chukua muda na wanafunzi wenzako kuyainua maombi yako mbele za Bwana, bila fadhaa na kwa moyo wa shukrani, ukizifanya haja zako (na sio madai yako!) zijulikane na Mungu. Ameahidi kwamba riziki na amani yake vitahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu (Flp. 4:6-7). Kumbukaneni ninyi kwa nyinyi katika siku za katikati ya wiki, na mchukulie kwa uzito maombi yenu na ya wengine, na mtaona jinsi Mungu anavyojibu maombi yenu kwa habari ya hekima, nguvu, na baraka zake. ~ Gareth Weldon Icenogle. Biblical Foundations for Small Group Ministry. (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1994.

Ushauri na Maombi Ukurasa wa 79  4

2

M A S O M O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker