Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

130 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

KAZI

Zaburi 1:1-3

Kukariri Maandiko

Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.

Kazi ya Usomaji

Kwa mara nyingine, hakikisha kwamba umekamilisha kazi ya usomaji uliopewa kama inavyoonyeshwa hapo juu, na kama ulivyofanya wiki iliyopita, tafadhali andika muhtasari mfupi kwa kila eneo ulilopewa kusoma. Leta muhtasari huo kwenye kipindi chetu kijacho (tafadhali tazama “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Pia, sasa ni wakati muafaka wa kuanza kufikiria kuhusu aina ya kazi ya huduma, na pia kuamua ni kifungu gani cha maandiko utakachochagua kwa ajili ya kazi ya ufafanuzi. Usichelewe kufanya maamuzi kuhusiana na kazi yako ya huduma na ya ufafanuzi. Kadiri utakavyofanya maamuzi hayo mapema ndivyo utajipatia muda wa kutosha wa kujiandaa na kutekeleza kazi zako. Katika somo letu linalofuata, Ushahidi wa Agano la Kale kuhusu Kristo na Ufalme Wake: Kutolewa kwa Ahadi , tutachunguza uhusiano kati ya Agano la Kale na Agano Jipya kupitia dhana ya ufunuo endelevu . Tutaangalia miunganiko ya ziada iliyopo katika Agano la Kale na Agano Jipya jinsi inavyohusiana na nafsi ya Kristo na Ufalme wake, na kuzingatia mada ya pekee ya ahadi na utimilifu , na jinsi mada hii inavyoliunganisha fundisho la Maandiko kuhusu Yesu Kristo na kulifanya kuwa moja. Umoja huu wa kweli unaonekana katika ahadi ya Mungu ya ajabu ya kutuma mkombozi kwa wanadamu ambaye kupitia kwake adui wa Mungu angeangamizwa, na wanadamu wangekombolewa. Katika protoevangelium (yaani, tangazo la kwanza la Injili katika Mwanzo 3:15), kupitia ahadi ya agano la Ibrahimu na mwendelezo wake tunaona jinsi tumaini la Kimasihi ndio kanuni unganishi ya Agano la Kale na utimilifu maridhawa wa Agano Jipya, huku kilele cha yote kikipatikana katika Yesu Kristo. Yeye ni uzao wa mwanamke na uzao wa Ibrahimu. Maandiko ya Kiebrania na yafunue utukufu wake kwetu, na kutugeuza tunapokuwa wanafunzi wenye bidii wa Neno takatifu la Mungu!

Kazi Zingine

2

M A S O M O Y A B I B L I A

Kuelekea Somo Linalofuata

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker