Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MUHTASAR I / 13

Utangulizi wa Mtaala wa Cornerstone , Toleo Rasmi la Ithibati

Karibu kwenye Mtaala wa Cornerstone , fursa yako mpya ya kuandaliwa kwa ajili ya huduma bora katika Kanisa!

Changamoto: Uhitaji Mkubwa, Hakuna Muda , Fedha Chache Ukweli mchungu anaoukabili mtu yeyote anayewaandaa wachungaji na wahudumu walei wanaotumika katika jamii zilizo hatarini, ni ule wa uhaba. Pesa na muda ni adimu na finyu sana kwa viongozi hawa hodari wanaomtumikia Mungu katika jamii maskini kuweza kujihusisha katika masomo ya muda marefu katika mfumo ulio rasmi. Wanafanya kazi isiyo ya kawaida huku mara nyingi wakiwa katika ajira za kudumu na wakipambania huduma inayokua. Maelfu ya wafanyakazi wa Kikristo walioko mijini ambao wangenufaika na mitaala yetu bora na yenye kina cha kiwango cha seminari kama Mtaala wa Capstone, hawana ama muda au fedha za kuikamilisha. (Muda wa wastani kwa wanafunzi wanaosoma na kufanya kazi kumaliza moduli kumi na sita za Capstone ni miaka mitatu hadi minne). Kukabiliana na Changamoto: Mtaala wa Cornerstone Ili kukabiliana na hitaji hili kuu, tumebuni mtaala huu wa kipekee, Mtaala wa Cornerstone. Ukiwa umechaguliwa kutoka kwenye masomo maalum ya kimkakati ya Capstone, na kuongezewa moduli ya “ Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini ” ya Dkt. Alvin Sanders, tuliunda kozi hii kwa ajili ya wale ambao hawana uhakika wa kuwa na muda au fedha za kukamilisha mtaala wetu mkubwa zaidi wa Capstone. Muda wa kukamilisha sehemu tatu za Cornerstone ni sawa na moduli tatu pekee za Capstone. Tuliunda nyenzo hii ili kuwasaidia wanafunzi hawa kuzifikia nyenzo muhimu pasipo kudhabihu ubora au fursa za huduma zao. Cornerstone itapunguza kwa kiasi kikubwa muda na gharama zinazohitajika kwa ajili ya shule ya kawaida ya Biblia au masomo ya seminari au hata Mtaala wa Capstone, pasipo kupoteza uaminifu wetu ama kwa Kweli ya kibiblia au kwa mafunzo ya huduma kwa vitendo. Kuandaliwa Kupanda, Kuchunga, na Kutumikia Kanisa! Nyenzo za mtaala wa Cornerstone zinajumuisha kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini na nyenzo zilizotolewa moja kwa moja kutoka kwenye moduli za Capstone, zikitoa kweli zake muhimu

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker