Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
14 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
kutoka kwenye maeneo manne ya idara zake (Masomo ya Biblia, Theolojia na Maadili, Huduma ya Kikristo, na Utume katika Miji). Tumeweka pamoja masomo ya Cornerstone ili kukupatia utaratibu thabiti wa mafunzo kwa wakati unaofaa na gharama nafuu. Mafunzo yetu yatakupatia ithibati, yataboresha ujuzi wako wa Maandiko, na kukuwezesha kuhudumu vyema kama mchungaji, kiongozi mlei, au Mkristo mtenda kazi mahali unapoishi na kufanya kazi. Mungu amekuita na kukupa karama, na tunatumaini kukuona ukitimiza wito wake kwenye maisha yako, ili upate kumletea heshima Mwokozi wetu katika kila jambo ulifanyalo. Kwa hiyo, ninakupa changamoto ya kutimiza huduma ya Bwana kwa ajili yako, yote katika nia ile ile kama ya Paulo anapomuasa Timotheo, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” (2 Tim. 2:15). Fahamu kwamba ukijitoa kwa Mungu kama mtu aliyekubaliwa, utatimiza wito wake na kuzaa matunda ya kiroho ambayo yatamtukuza Kristo na kumpendeza Mungu. Mungu akubariki sana katika masomo yako, ufuasi wako, na huduma yako! Kwa ujasiri mkubwa katika Neno la Mungu la milele lenye kuponya
na kubadilisha, Dkt. Don Davis Wichita, Kansas Februari 1, 2023
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker