Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MUHTASAR I / 15

Maelezo ya Kozi

Mtaala wa Cornerstone ni mafunzo ya hali ya juu kwa viongozi wa Kikristo ambao huenda wasihitaji au wasiwe na muda wa kupata mafunzo ambayo huchukua miaka kadhaa. Mtaala huu unatoa maarifa na ujuzi kuhusu uongozi wa Kikristo katika muundo mfupi. Mafunzo haya bora yanajumuisha sehemu kuu tatu. Sehemu ya I: Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini inatoa mtazamo mpya wa jinsi ya kuwawezesha wale wanaoishi katika hali ya umaskini. Wanafunzi wanapata nafasi ya kuchunguza mawazo yao kuhusu wale wanaoishi katika hali ya umaskini na kujifunza jinsi ya kufanya kazi ya kimungu na yenye matokeo kati yao. Sehemu ya II: Biblia na Theolojia Fungu la Mafunzo ya Biblia linalenga kuwaandaa wanafunzi kuhudumia Neno la Mungu kwa usahihi na ufanisi. Mtumishi wa Kristo lazima awe na umahiri katika mambo yaliyomo katika Biblia, ajinyenyekeze kwa maagizo yake, na afundishe kweli yake. Fungu la Theolojia na Maadili linalenga kuwaandaa wanafunzi kueleza na kutetea kweli za msingi za Imani ya Kikristo. Somo alilopenda zaidi Yesu mwenyewe lilikuwa Ufalme wa Mungu. Ulikuwa ni ujumbe wake wa wokovu, mpango mkuu, na theolojia yake pendwa. Sehemu hii inaangazia hadithi ya ufalme – Mfalme na Ufalme wake – na kuona umuhimu wake katika maisha ya ufuasi binafsi na huduma. Sehemu ya III: Huduma & Umisheni Fungu la Huduma ya Kikristo linalenga kuwaandaa wanafunzi kuchunga kwa ustadi kundi la Mungu, yaani Kanisa. Yesu wa Nazareti ameinuliwa kama kichwa juu ya watu wake wapya, Kanisa. Tunazingatia jukumu muhimu la Kanisa katika ufuasi binafsi na wa jumuiya. Hakika, hakuna ufuasi au wokovu nje ya kazi ya Mungu ya kuokoa kupitia Kanisa. Fungu la Utume katika Miji linalenga kuwaandaa wanafunzi kumwakilisha Kristo kama mabalozi wa Ufalme wake. Tunazingatia imani ya Kikristo kama mwitikio wa utume, wito wa kwenda kwa mataifa na kumtangaza Yesu wa Nazareti kama Bwana na Mfalme wa utawala wa Mungu.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker