Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 133

Ushahidi wa Agano la Kale kuhusu Kristo na Ufalme Wake Kutolewa kwa Ahadi

S OMO L A 3

Ukurasa wa 81  1

Karibu katika jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya nyenzo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kufafanua uhusiano kati ya Agano la Kale na Agano Jipya kupitia wazo la ufunuo endelevu , ambalo linathibitisha kwamba Mungu amejifunua hatua kwa hatua na kwa uhakika katika historia ya watu wake, na hatimaye kupitia Yesu Kristo. • Kuainisha vipengele mbalimbali vya ufunuo endelevu , ambavyo ni pamoja na ufunuo endelevu wa Mungu kwetu kupitia uumbaji, kupitia madhihirisho na matukio maalum, na katika siku hizi za mwisho kupitia Mwanawe. • Kuonyesha jinsi Agano la Kale linavyofafanua na kufunua Agano Jipya kupitia nafsi ya Kristo, na jinsi maagano yote mawili yanavyolenga ufunuo wa mwisho na kamili wa Mungu juu yake mwenyewe katika Yesu Kristo na utawala wa ufalme wake. • Kuelezea usemi wa Agustino kuhusu uhusiano kati ya maagano mawili: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.” • Kuangazia dhana kamilishi zinazounganisha na kuelezea uhusiano wa Agano la Kale na Jipya, ikijumuisha Agano la Kale kama linalotoa utangulizi wa hitimisho la Agano Jipya kuhusu Kristo, Agano la Kale kama matarajio ya Kristo na Agano Jipya kama kilele chake, Agano la Kale kama kivuli cha Kristo na kazi yake na Agano Jipya kama utimilifu wa kivuli hicho, Agano la Kale kama ufunuo wa awali na hafifu wa wokovu wa Mungu na ufunuo wa Agano Jipya katika Kristo kama ukamilifu mkuu wa ufunuo huo, na Agano la Kale kama namna maalum ya wokovu wa Mungu, ambao umefanyika kuwa wa mataifa yote katika Agano Jipya. • Kutoa ufafanuzi na vipengele vya mada ya ahadi na utimilifu katika ufunuo wa Agano la Kale, ambayo inathibitisha ahadi ya Mungu kwa mteule wake mwenyewe kuwakomboa wanadamu na kuharibu kazi ya shetani, ahadi iliyotimizwa katika nafsi ya Yesu wa Nazareti.

Malengo ya Somo Ukurasa wa 84  2

3

M A S O M O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker