Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
134 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
• Kutambua vifungu vikuu katika Maandiko ambavyo vinathibitisha jinsi kazi ya Agano la Kale inavyotoa ushuhuda wenye mvuto na wa uhakika kwa habari ya Masihi, uliotimizwa katika Yesu Kristo (rej. Luka 22:25-27, 44-48; Mt. 5:17-18; Mt. ; Yoh 1:45; 5:39-40; • Kuelezea maana za mada ya ahadi na utimilifu kwa ajili ya uchambuzi wa Agano la Kale, hasa jinsi inavyoonyesha kwamba taswira ya wazi ya Masihi inaweza kuonekana katika historia ya mababa wa kale, taifa la Israeli, unabii wa Kimasihi, na viwango vya maadili vya Sheria. • Kuorodhesha njia ambazo mada ya ahadi na utimilifu inathibitisha umoja wa Agano la Kale na Agano Jipya, katika suala la nia ya Mungu kujidhihirisha mwenyewe, kuwakomboa watu wake, na kufanya hivyo kupitia ahadi iliyotolewa kwa Ibrahimu na uzao wake, iliyotimizwa kupitia Yesu wa Nazareti. Mtimiza Ahadi kwa Asili Mwa. 3:15 – nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Je, unatimiza ahadi zako, au unabadilika na kukana kile ulichoahidi kufanya? Kundi fulani la wanaume maarufu limejipa jina la “Watimiza Ahadi,” likiainisha maeneo saba ambayo wanachama wake huweka nadhiri kwa Bwana na kila mmoja kwa mwenzake kwa habari ya uaminifu wao kwa Mungu na kwa Ufalme wake. Wazo la ahadi ni wazo muhimu katika jamii yetu, iwe ni katika dhana zetu za kawaida za mapenzi ya uchumba, “Nimejiahidi kwa Sherri,” au hati za ahadi na makubaliano zinazohusiana na biashara na masuala ya kisheria. Kwa kweli, wazo la ahadi ni wazo muhimu katika mahusiano yetu yote ya siku za leo: ahadi hutolewa kati ya mataifa, viongozi wa dunia, majeshi, washirika wa kibiashara, wanafamilia na wakandarasi. Bila dhana ya kutoa na kutimiza ahadi, mifumo yetu yote ya kijamii isingeweza kufanya kazi. Mojawapo ya njia rahisi na ya moja kwa moja ya kuielewa hadithi ya Biblia ni dhana ya ahadi na utimilifu wake. Kwa namna moja Biblia katika ukamilifu wake inaweza kuonekana kuwa ni harakati za Mungu mwenye enzi kuu, Mungu wa Israeli, Yehova, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye anatoa ahadi kwa wanadamu wawili wa kwanza walioasi na nyoka aliyemdanganya Hawa. Katika andiko hili Mungu anatoa ahadi itakayomwathiri nyoka na uzao wa mwanamke. Katika duru za kitheolojia ahadi hii inaitwa “ protoevangelium ,” kutajwa au kusimuliwa kwa mara ya kwanza kabisa kwa ujumbe wa Injili ya wokovu wa wanadamu
Ibada Ukurasa wa 84 3
3
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker