Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 135

unaopatikana katika Biblia. Hapa Mungu anaweka mpango mzima wa wokovu katika kifungu kifupi kinachotoa muhtasari wa mojawapo ya mawazo muhimu sana katika Maandiko. Mazingira ya tukio hili katika kifungu hiki ni wakati ule wa kusikitisha ambapo watu wawili wa kwanza, Adamu na Hawa, wananaswa katika tendo lao la aibu la kukubali kula tunda la Mt iwa ujuzi wa Mema na Mabaya, kinyume cha amri ya moja kwa moja kutoka kwa Bwana. Nyoka, ambaye alimdanganya Hawa katika tendo lake la uasi, Hawa, na Adamu wote wako mbele ya Bwana ambaye analeta hukumu yake juu yao. Katika kuzungumza na nyoka, Mungu anatoa tangazo kuhusu wakati ujao, tangazo ambalo kiuhalisia linalifanya andiko hili kuwa mwanzo wa mwisho wa ufunuo wote wa Maandiko ulioandikwa. Hapa Mungu asema wazi wazi kwamba kusudi lake kuu kwa nyoka litakuwa uadui wa kudumu na usioisha kati ya nyoka na uzao wa mwanamke, kati ya uzao wa nyoka na ule wa mwanamke. Nyoka angeponda kisigino cha “Uzao” wa mwanamke, lakini uzao huo wa mwanamke ungeponda kichwa kizima cha nyoka. Picha hii ya wazi ya nyoka na uzao wa mwanamke ndio kiini cha maono ya wokovu katika Biblia. Mungu anasema kwamba kwa sababu ya uasi huo wa hiari wa wanadamu, ameanzisha aina ya mahusiano katika ulimwengu ambayo yatakuwapo daima, uadui usiokoma kati ya nyoka na uzao wa mwanamke, kati ya uzao wake na ule wa mwanamke. Kutokana na usomaji wa awali wa andiko hili, wasomi wa Kiyahudi waliona kuwa ni kutajwa kwa kwanza kwa ahadi ya kimungu kwa habari ya Masihi, uzao huu, mtu huyu ambaye angetokana na mwanamke na bado angeleta ukomo wa utendaji wa nyoka na uongo, udanganyifu, na nia mbaya iliyolaaniwa dhidi ya jamii ya wanadamu. Tunajua kwamba ahadi hii ilirudiwa kwa Ibrahimu ambaye aliahidiwa kuwa uzao wake ungebarikiwa na ungekuwa baraka kwa mataifa yote (Mwa. 12-13). Ahadi hii ya uzao, mrithi, shujaa aliyebarikiwa ambaye angemaliza kazi za ibilisi, ilirudiwa tena kwa wana wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, na kisha kwa mwana wa Yakobo, Yuda (Mwa. 49). Ahadi hii inaendelea katika Agano la Kale, kupitia nyumba ya Yuda, hadi inawekwa wazi kwamba mzao huyu angekuwa mrithi wa nyumba ya Daudi (taz. 2Sam. 7), na manabii wanaongezea rangi zaidi, ujuzi, na ufunuo kuhusu tabia na kazi ya mzao huyu (k.m., Isa. 9:6-7; 53:1-12). Hatimaye, mzao huyo anafunuliwa katika Agano Jipya kuwa ni Yesu wa Nazareti, ambaye yeye mwenyewe ni utimilifu wa ahadi ya kale ya Bwana kuleta duniani mtu ambaye angewakomboa watu wake, kurejesha uumbaji, na kutawala milele kama Bwana na Mfalme wa ulimwengu wa Mungu. Mitume wanaweka wazi kwamba Yesu wa Nazareti kwa kweli ndiye mzao wa Ibrahimu aliyengojewa kwa muda mrefu (kama asemavyo Paulo katika Wagalatia 4:4, “Hata

3

M A S O M O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker