Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
136 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria”). Vivyo hivyo, Yohana anaweka wazi kusudi la Yesu wa Nazareti kuja ulimwenguni: 1 Yohana 3:8 “atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” Kweli, Yesu wa Nazareti ni utimilifu wa ahadi ya kale ambayo Yehova aliahidi kutuma, kupitia uzao wa wanadamu, mzao wa mwanamke, mtu ambaye angewakomboa wanadamu kutoka katika hatia yao, na hatimaye kuharibu kazi za ibilisi. Picha hii ya nyoka ambaye kichwa chake kimepondwa na shujaa mshindi wa Bwana inatawala katika taswira na usemi wa mitume. Zingatia mada zifuatazo katika vifungu vya Maandiko ya AJ hapa chini: Rum. 16:20 – Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]. Efe. 4:8 – Kwa hiyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. Kol. 2:15 – akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo. Ebr. 2:14-15 – Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 1 Yoh. 3:8 - atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 1 Yoh. 5:5 – Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? Maandiko haya na mengine yanatueleza kuhusu nguvu ya ahadi ya Bwana ya “kuponda kichwa cha nyoka” kupitia “mzao wa mwanamke” aliyemchagua mwenyewe na kumpaka mafuta. Mungu ameamua kuunganisha historia nzima ya wanadamu na utimizo wa ahadi moja ambayo alitoa kuhusu urejesho na ukombozi wa uumbaji wake kupitia Yesu wa Nazareti. Sasa tunajua kwamba ahadi hii kwa sehemu tayari imetimizwa katika ujio na kazi ya Yesu wa Nazareti, na hivi karibuni atakamilisha kazi yake aliyoianza msalabani wakati wa Kuja kwake Mara ya Pili. Je, haishangazi kwamba historia yote ya dunia nzima na ulimwengu wote inaweza kuhusishwa na ahadi moja na azimio kamili la Mungu wetu mkuu na mwaminifu kutimiza Neno lake? Huu ndio msingi wa imani yetu, moyo wa ibada yetu, na msingi wa
3
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker