Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 137

usomaji wetu wa Maandiko. Ahadi hii ya kimungu ilipitia historia takatifu ya watu wa Israeli hadi ilipotimizwa katika nafsi ya Yesu wa Nazareti. Yeye ndiye kiini na mwisho wa kazi yote ya wokovu ambayo Mungu anaifanya katika ulimwengu huu. Je, haishangazi kwamba Mungu wetu, Mungu huyu mkuu, ni Mungu wa ahadi ambaye aliitimiza kwa njia ya Yesu Kristo? Je, si jambo la kustaajabisha kujua kwamba yule aliyetuahidi hatabadili mawazo yake kamwe, bali atatimiza ahadi yake takatifu, kwa utukufu wa jina lake, na ajili ya wokovu wa watu wake? Hebu tutangaze imani yetu katika uthibitisho rahisi wa ahadi ya mtume, na tuishi kama watu tunaoiamini kwa mioyo yetu yote na akili zetu zote. 1 Thes. 5:23-24 – Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya. Mungu aliyeweka kusudi lake kuu kwa ulimwengu katika bustani, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa hakika, yeye ndiye Mtimiza Ahadi kwa Asili!

Baada ya kutamka na/au kuimba ukiri huu wa imani (taz. Kiambatisho) omba maombi yafuatayo:

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

3

Ee Mungu wa milele na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, utujalie neema yako ili tuweze kusoma Maandiko Matakatifu kwa bidii, na, kwa mioyo yetu yote, kumtafuta na kumpata Kristo ndani yake, na kupitia kwake tupate uzima wa milele; kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Amina.

M A S O M O Y A B I B L I A

~ John W. Doberstein, mh. A Lutheran Prayer Book. Philadelphia: Fortress Press, 1960. uk. 102.

Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita, yaani Zaburi 1:1-3.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukusanya

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker