Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
138 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
KUJENGA DARAJA
Kuna Uwezekano kwamba Tunatumia Kitabu Sahihi kwa Namna Isiyo Sahihi? Mojawapo ya masuala yanayoendelea na matatizo yanayohusiana na umilisi wa Agano la Kale ni namna litavyotumiwa vibaya na wafasiri wengi, wahafidhina na huria. Agano la Kale ni maktaba yenye fasihi tofauti tofauti kiasi kwamba wasomi wengi wa Agano la Kale hawatafuti tena kutupatia theolojia ya Agano la Kale inayoakisi umoja wa Maandiko hayo. Badala ya umoja, Maandiko ya Agano la Kale yanaonekana kama yaliyohaririwa sana (yaliyorekebishwa) na ambayo yanahusu karne nyingi, waandishi kadhaa, na yasiyotoa ujumbe thabiti na wenye muunganiko kwa mfasiri. Hata kwa Wakristo wengi wa kiinjili, Biblia inasalia kuwa kitabu kilichofungwa. Kimsingi, inatumiwa kwa ajili ya usomaji wakati wa ibada ambapo Zaburi na Mithali husomwa, huku sehemu kubwa za Agano la Kale zikibaki bila kuhubiriwa wala kusomwa na waumini wengi wa kiinjili. Je, ni sababu gani ambayo watakatifu hawa wapendwa wanaoipenda Biblia wanazitoa zinazowapelekea kulipuuza kabisa Agano la Kale? Ni ngumu sana kulielewa na kulitumia. Ni mara chache sana wanatokea kufanya rejea ya Maandiko ya AK kwa sababu hayaeleweki, yamejaa vifungu vigumu, na yamejikita sana katika sehemu za sheria za kiibada na/au vivuli na taswira. Kwa kweli, kwa Mkristo mpya au anayekua ni rahisi zaidi kuzingatia Agano Jipya na kusoma Nyaraka, na, ikiwa mtu ana ujasiri wa kutosha, ataenda kwenye Injili na kusoma maneno ya Bwana. Lakini, katika suala la ufahamu na kutamanika, Wakristo wengi wanashuhudia kwamba Agano la Kale si sehemu muhimu ya safari zao za kiroho. Je, unafanya nini kuhusu hali hii, na kupuuzwa kwa Agano la Kale kunajidhihirishaje katika uzoefu wako? Katika nyakati hizi zilizojaa harakati za kudai ustahimilivu na kuchukuliana na watu wenye mitazamo na itikadi tofauti, nyakati za usahihi wa kisiasa, na hisia za kinyongo na chuki dhidi ya jambo lolote ambalo linaashiria kuleta hukumu au adhabu, Agano la Kale ni kitabu ambacho kimeandamwa na kukashifiwa sana. Kwa kweli, limejaa hadithi nyingi zinazohusisha taswira zote za giza za maisha ya mwanadamu, na inajumuisha maonyesho ya wazi ya mauaji, ubakaji, vurugu, vita, na misiba. Mifano ya hukumu kali inatolewa katika hadithi nyingi, na watu wenye imani na mitindo fulani ya maisha isiyokubalika sio tu kwamba wanahukumiwa kimaadili, lakini kwa undani na kwa kina tunawaona wakihukumiwa na jamii na Mungu mwenyewe. Kauli za Mungu dhidi ya chaguzi kadhaa za mitindo ya maisha ya kisasa zimelifanya Agano la Kale hasa kuwa kiini cha mijadala na mabishano mengi. Baadhi ya Wakristo Je, Mungu wa Agano la Kale ndiye Mungu Yule Yule wa Agano Jipya?
1
Ukurasa wa 87 4
3
M A S O M O Y A B I B L I A
2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker