Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | USHAHIDI WA AGANO J IPYA KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUPINGWA KWA MASIHI / 159
Ushahidi wa Agano Jipya kuhusu Kristo na Ufalme Wake Kupingwa kwa Masihi
S OMO L A 4
Ukurasa wa 93 1
Karibu katika jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya nyenzo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea kwa kina dhana ya Kiyahudi la Ufalme wa Mungu wakati wa Yesu, iliyochochewa na ukandamizaji waliokuwa wakiupitia kutoka kwa mamlaka za dola, ikijumuisha imani yao kwamba Ufalme wa Mungu utakuja kwa nguvu, kuleta urejesho wa ulimwengu unaoonekana na kuokoa wanadamu kutokana na udhibiti wa Shetani. • Kutoa utetezi juu ya ushahidi wa kibiblia unaounga mkono wazo la kwamba Yesu alitangaza Ufalme uliopo, na kudhihirisha uhalisia wa Ufalme huo kupitia maisha yake na kazi za uponyaji na kutoa pepo. Mtumishi na BwanaWake Soma Yohana 15:18-26 . Je, mwanafunzi wa Yesu anaweza kuishi katika ulimwengu huu pasipo kupitia aina ya kukataliwa, kuteswa, na dhiki ambayo Bwana wetu aliipitia? Je, uzoefu wa Bwana wetu ulikuwa sui generis (mahususi kabisa) kwake tu, au lazima watu wote walio wake pia wapitie kiwango cha chuki na kukataliwa na ulimwengu kama Yeye? Mojawapo ya maneno aliyoyapenda sana Yesu ni neno hili lililojulikana sana, “Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.” (Yohana 13:16). Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyemtuma. Yesu, Bwana mkuu kwelikweli na mwenye enzi yote, alivumilia mateso na chuki ya watu wasiomcha Mungu na wenye mioyo migumu, na neno lake la wazi katika andiko letu la ibada ni kwamba ikiwa ulimwengu ulimchukia, utatuchukia sisi pia. Hakuna mfuasi wa kweli wa Yesu anayeweza kupita katika ulimwengu huu bila makovu, bila upinzani, akifanya kazi kwa utukufu bila kujeruhiwa wala kuumizwa; sisi sote lazima tupitie kukataliwa na upinzani wa maadui wa Mungu. Tunapaswa kupambana, tutapingwa, hata kuchukiwa, kwa ajili ya Kristo. Hatuhitaji kustaajabia hili, hata hivyo. Yesu mwenyewe, Bwana na Mwalimu wetu, alikataliwa na kuchukiwa, kadhalika na sisi, kwa sababu ya muungano wetu naye, tutapitia hali hiyo hiyo. Mungu atawapa wale walio wa Kristo neema ile ile aliyopokea,
Malengo ya Somo Ukurasa wa 96 2
Ibada Ukurasa wa 96 3
4
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker