Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

160 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

ambayo ilimwezesha Bwana wetu kustahimili chuki na unyanyasaji huo kwa ajili ya Baba. Kila wakati, unapostahimili taabu na majaribu, dhiki, chuki, na shida, kumbuka kwamba Bwana wetu alivumilia hayo, na atatusaidia kuvumilia hadi mwisho. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni Imani ya Nikea (iliyo katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu Mwenyezi, Wewe ambaye Mwanao aliyebarikiwa aliongozwa na Roho kujaribiwa na Shetani: Njoo upesi utusaidie sisi tunaoshambuliwa na majaribu mengi; na, kama unavyojua udhaifu wa kila mmoja wetu, basi kila mmoja akuone wewe ni hodari wa kuokoa; kwa Yesu Kristo Mwanao Bwana wetu, anayeishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, sasa na hata milele. Amina.

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

~ Episcopal Church. Kitabu cha Maombi ya Pamoja na Utoaji wa Sakramenti na Ibada Nyingine

na Sherehe za Kanisa, Pamoja na Zaburi au Zaburi ya Daudi. New York: The Church Hymnal Corporation, 1979. uk. 218.

Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita, yaani Luka 24:44-48.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

4

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukusanya

M A S O M O Y A B I B L I A

KUJENGA DARAJA

Je, Injili Inayoahidi Afya na Utajiri ni Potofu? Wengi sasa wanatangaza injili ambayo inaahidi urahisi wa maisha, faraja, na baraka katika ulimwengu unaozidi kujaa machafuko, ubaya na ukosefu wa haki. Kiini cha injili hii ni imani kwamba kifo cha Yesu kilimletea mwamini ushindi ambao unagusa kila eneo la maisha bila kuacha doa lolote au mchanganyiko wa shida au majaribu. Tukiwa na imani thabiti, ikiwa ukiri wetu uko wazi, na uthibitisho wetu wa Neno la Mungu ukiwa thabiti, tutapokea afya na mali kutoka kwa Bwana, yaani baraka zinazowajia wale ambao imani yao inabaki kuwa imara, isiyoyumba na yenye nguvu. Mtindo huu wa maisha ya baraka na ushindi ni kiashiria cha imani inayookoa;

1

Ukurasa wa 98  4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker