Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | USHAHIDI WA AGANO J IPYA KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUPINGWA KWA MASIHI / 161
wale wanaoshikamana na Mungu wanahakikishiwa kiwango cha baraka na neema ambayo haitapungua, maadamu imani yao inabaki thabiti. Unaamini nini kuhusu “injili” hii? Je, ni ya kibiblia, ya kupita kiasi, au hata ya kizushi?
Swali kwa habari ya Majiji: Aina za Mateso Katika vitongoji vya mijini siku hizi ni dhahiri kwamba watu wengi wanateseka kila siku kwa sababu ya taabu na shida nyingi. Wengine wamekosa makazi na chakula, hawana makao wala mavazi, au wana uhitaji wa mahitaji ya msingi ya maisha na matibabu kwa ajili ya afya zao. Wengi ni wahasiriwa wa dhuluma na jeuri, na wengine huishi kila siku katika upweke na kukata tamaa. Je, nafasi ya taabu ni ipi katika maisha ya Kikristo? Kwa nini mambo ya kutisha yanatokea kwa baadhi ya watu bora zaidi, na baadhi ya watu waovu zaidi na wasio waadilifu wanaonekana kuishi maisha yasiyo na matatizo? Je, kuna aina tofauti za taabu; kuna aina ya taabu na upinzani ambao kwa hakika unawaongoza watu wa Mungu katika utauwa na kukua kiroho na kiimani, au je, aina zote za taabu ni matokeo ya dhambi na chuki ya adui kwa watu wa Mungu? Alaumiwe Anayestahili Kulaumiwa Ni nani hasa wa kulaumiwa kwa upinzani na chuki ambayo mara nyingi hutokea katika maisha ya wale walio wa Yesu? Ingawa ni dhahiri kabisa kwamba Yesu alikabili upinzani kutoka pande mbalimbali si kwa sababu yake mwenyewe bali kwa nia mbaya ya adui zake, je, sisi pia tunaweza kusema hivyo? Je, sisi kama wanafunzi wa Yesu tunapata upinzani kwa sababu ya ushirika wetu na yeye, au nyakati fulani tunapata upinzani kwa sababu ya dhambi zetu wenyewe na matendo yetu yasiyo ya kimungu kwa wengine? Ikiwa hiyo ni kweli, basi tunawezaje kutambua kwamba tunapata mateso kwa sababu ya utii wetu kwa Yesu, au kwamba mateso yanatokana na tabia zetu za dhambi katika ulimwengu huu?
2
3
4
M A S O M O Y A B I B L I A
Kupingwa kwa Masihi Upinzani kutoka kwa Nguvu za Giza
Mch. Dr. Don L. Davis
MAUDHUI
Ingawa dhana ya Kiyahudi kuhusu Ufalme wa Mungu nyakati za Yesu ilisisitiza utukufu wa Israeli na kushindwa kwa Mataifa, Yesu alikuja akitangaza Ufalme wa Mungu kama uliopo na unaoonekana katika nafsi yake na kazi zake. Katika utu wa Yesu wa Nazareti,
Muhtasari Ukurasa wa 98 5
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker