Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

162 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Ufalme wa Mungu uliokuwa ukingojewa kwa muda mrefu ulikuwa umefika, lakini si kwa njia ambayo Wayahudi walikuwa wametabiri na kutarajia. Hata hivyo, katika nafsi yake na kupitia matendo yake mema ya miujiza, Yesu alitangaza Ufalme kama jambo la sasa, na alionyesha uhalisia wake katika uponyaji wake na kutoa pepo. Lengo letu la somo hili, Kupingwa kwa Masihi: Upinzani kutoka kwa Nguvu za Giza , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Dhana ya Kiyahudi ya Ufalme wa Mungu wakati wa Yesu ilikuwa na mizizi katika nguvu na utukufu wa taifa la Israeli, na tumaini la Israeli kuzishinda mamlaka za Mataifa yaliyokuwa yakiwakandamiza. • Dhana hii ya Kiyahudi ilimwelewa zaidi Masihi kama ambaye angekuja katika uwezo mkuu na wa kutisha, akirejesha Ufalme wa Mungu katika ulimwengu unaoonekana, na katika wakati mgumu wa wokovu angewakomboa wanadamu kutoka katika udhibiti wa Shetani. • Maoni ya Yesu kuhusu Ufalme yalipingana na watu wa siku zake kwa sababu Yesu alitangaza Ufalme kuwa ndani yake mwenyewe na kazi zake za nguvu, jambo lililoonyeshwa katika uponyaji wake na kutoa pepo. • Kama Masihi halisi – ingawa hakutarajiwa wala kusadikika kuwa ndiye – Yesu alizipinga zile nguvu za kiroho ambazo zimeushikilia ulimwengu na jamii ya wanadamu mateka tangu anguko. • Yesu wa Nazareti anatimiza ahadi ya ufalme, na kwa hiyo kama Masihi anayakabili madhara ya laana na kupambana na kazi za ufalme wa giza.

4

M A S O M O Y A B I B L I A

I. Usuli wa Dhana ya Kiyahudi ya Ufalme wa Mungu

Muhtasari wa Maudhui ya Video

A. “Ufalme” katika ulimwengu wa kale

1. “ Ufalme ” wakati wa Yesu katika eneo hilo ulimaanisha “ubwana,” “utawala,” “mamlaka,” au “enzi kuu.”

2. Ukuu wa Mungu au Utawala wa Mungu = Ufalme wa Mungu

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker