Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

UTANGUL I Z I WA FUNGU LA THEOLOJ I A NA MAAD I L I / 181

Utangulizi wa Fungu la Theolojia na Maadili

Salam, katika jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Karibu kwenye fungu la pili la Mtaala wa Cornerstone, Theolojia na Maadili . Kati ya mambo yote yaliyohubiriwa na kufundishwa na Yesu wa Nazareti, hakuna somo lolote lililo muhimu na lenye mvutano kama habari ya Ufalme wa Mungu. Wasomi wote wa kihafidhina na waliberali wanakubali kwamba somo alilopenda zaidi Yesu, ambalo alihubiri na kufundisha mara nyingi zaidi, ni Ufalme wa Mungu. Ulikuwa ni ujumbe wake wa wokovu, mpango mkuu, na theolojia yake pendwa. Cha kusikitisha ni kwamba, Kanisa la kisasa linaonekana kutozingatia sana kile ambacho Yesu alikiona kuwa chenye umuhimu zaidi katika huduma yake ya kinabii na ya Kimasihi. Imani yetu ni kwamba moyo wako utashikwa na hadithi ya ufalme – Mfalme na Ufalme wake – na kuona umuhimu wake katika maisha yako ya ufuasi binafsi na huduma. Katika somo letu la kwanza, Ufalme wa Mungu: Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu , tutaangazia nia ya Mungu ya kuondoa uasi wote na kutokutii kama matokeo ya Anguko – Mungu anakuwa Shujaa katika ulimwengu huu ulioanguka. Yesu wa Nazareti ni uwepo wa Ufalme unaotimizwa, huku utawala wa Mungu ukidhihirishwa katika kuvaa kwake mwili, kifo, ufufuo, na kupaa kwake. Hadithi ya Ufalme ni hadithi ya Yesu, na nia ya Mungu ni kurudisha ulimwengu chini ya utawala wake ndani yake. Tunamsifu Mungu kwa hadithi yake ya ufalme, na shauku yako kama mwanafunzi wa Neno lake Takatifu! Elimu kuhusu Mungu wetu, Baba Mwenyezi, ni mojawapo ya elimu zenye utajiri mkubwa sana katika Neno la Mungu. Inaathiri kila sehemu ya ufuasi wetu, ibada, na huduma; Kwa kweli, kama Bwana wetu Yesu alivyosema, “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana 17:3). Katika somo letu la pili, Mungu Baba: Mungu katika Utatu – Ukuu wa Mungu , tutaangalia ushahidi wa kibiblia hukusu Utatu, Nafsi tatu za Mungu. Maandiko yanafundisha kwamba kuna Mungu mmoja tu, na bado Mungu huyuhuyu anajidhihirisha kama Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Washiriki wa Utatu wako katika umoja, utofauti na usawa, Mungu mmoja wa kweli, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Hakika, Mungu wetu Baba Mwenyezi ndiye Mungu wa mbinguni mmoja, wa kweli na wa utukufu. Kumjua vizuri zaidi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker