Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

182 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

kutatusaidia kumwakilisha kwa heshima tukiwa watumishi wake. Mungu akubariki unapochunguza utajiri usioelezeka wa Maandiko kuhusu Mungu wetu mkuu na mwenye nguvu! Utambulisho wa Yesu wa Nazareti na kazi yake ni somo muhimu katika tafakari na huduma zote za Kikristo. Hakika, haiwezekani kuhudumu katika jina la Bwana Yesu Kristo ikiwa huduma hiyo imejengwa juu ya mtazamo potofu na wa aibu kuhusu yeye alikuwa nani (na ni nani), maisha yake yalimaanisha nini, na kile tunachopaswa kufanya kwa ajili yake leo. Mtazamo sahihi juu ya maisha yake, kifo, ufufuo, kupaa, na kurudi kwake ndio msingi wa kila kitu katika maisha, imani na huduma tuifanyayo. Katika somo letu la tatu, Mungu Mwana: Yesu, Masihi na Bwana wa Wote – Alikufa tutachunguza maana za kitheolojia za unyonge na kifo cha Yesu, kushuka kwake katika utu wake wa kiungu kwa niaba yetu. Tutaangazia kunyenyekezwa kwa Yesu kwa njia ya Umwilisho (incarnation) , maisha na huduma yake, pamoja na kifo chake. Katika kuzingatia dhabihu yake pale Kalvari, tutachunguza baadhi ya mifano ya kihistoria inayosaidia kuelewa kazi yake juu ya msalaba. Hii inahusisha mtazamo wa kifo chake kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho (utoshelevu wa kimungu) kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Pia tutachunguza baadhi ya maoni mbadala ya kihistoria kuhusiana na kifo cha Yesu. Haya ni pamoja na kifo chake kama 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. Huenda hakuna fundisho linaloweza kulinganishwa na msisimko unaotokana na kuelewa kwa njia ya kibiblia na ya kiimani utajiri, ajabu, na fumbo la Mwana wa Mungu, Yesu wa Nazareti. Kufedheheshwa kwake na kupaa kwake ndicho kiini cha Injili, na kitovu cha uchaji, ibada na huduma yetu. Mungu atumie somo hili kuhusu mtu wake mtukufu kukuwezesha kumpenda zaidi na kumtumikia yeye ambaye pekee ndiye aliyepewa ukuu na Baba. Kuna kweli chache za kitheolojia katika historia ya Kanisa ambazo zimezua mabishano mengi, kutokubaliana, na mafarakano kama fundisho la Roho Mtakatifu. Kuanzia mabishano ya zamani kuhusu Utatu na fundisho la “procession” (yaani fundisho kuhusu nafsi ipi ya Utatu iliipeleka nafsi nyingine kutenda kazi) hadi kutokubaliana kwa siku za leo kuhusiana na ubatizo na karama za Roho Mtakatifu, kuna mengi ambayo yanaweza kutufanya tuliendee somo hili kwa tahadhari; lakini, ninatumai kwa dhati kwamba haitakuwa hivyo. Fundisho la Roho Mtakatifu ni kiini cha uelewa wetu kuhusu asili ya Mungu na namna tunavyoweza kuuishi uwepo wake hai katikati yetu. Roho ametumwa ili kulitia nguvu na kuliongoza Kanisa la Mungu na kuwapa maisha mapya wale wote wanaoitikia kwa imani ujumbe wake kuhusu Yesu. Ni imani yetu kwamba ukweli

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker