Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
UTANGUL I Z I WA FUNGU LA THEOLOJ I A NA MAAD I L I / 183
unaojifunza kuhusu Roho Mtakatifu hautakuwa tu “theolojia rasmi” ambayo inakusaidia kumwelewa Mungu vizuri zaidi, lakini pia itakuwa “theolojia ya vitendo” ambayo inakuwezesha kumtegemea Roho Mtakatifu katika kiwango kinachoongezeka daima kwa kadri unavyoendelea kuhudumu katika Kanisa la Mungu na kushuhudia ulimwenguni. Somo la nne, Mungu Roho Mtakatifu: Nafsi ya Roho Mtakatifu , linalenga kujifunza kuhusu Mungu Roho kama nafsi ya tatu ya Mungu mmoja wa Utatu. Tutazungumza kuhusu Roho kama “Mpaji wa Uhai” na kuonyesha jinsi majina, vyeo, na alama za Roho katika Maandiko zinavyomwonyesha yeye kama chanzo na mtegemezaji wa maisha ya kimwili na ya kiroho na kama nafsi iliyo kazini ili kuvifanya vitu vyote kuwa vipya. Nafsi ya Roho Mtakatifu ni halisi na muhimu kama Mungu Baba na Mungu Mwana. Roho ametumwa na Baba na Mwana ulimwenguni ili tuweze kupata ushirika wa upendo pamoja nao na ili tuweze kutiwa nguvu kutii amri za Mungu na kutimiza utume wake. Ombi letu ni kwamba viwango vyenu vya kumtegemea Roho vitakua mnapojifunza Maandiko pamoja.
Kazi katika Fungu Hili Kama sehemu ya ushiriki wako katika Mtaala wa Cornerstone, utahitajika kufanya ufafanuzi (uchambuzi wa kina) wa kifungu kimojawapo katika Neno la Mungu:
Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko
a. Luka 11:15-23 b. Isaya 40:22-26 c. Wafilipi 2:5-11 d. Warumi 8:13-25
Kusudi la kazi hii ya ufafanuzi wa Maandiko ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kifungu mojawapo mihimu kuhusu asili na kazi ya Neno la Mungu. Unaposoma mojawapo ya vifungu vilivyopo hapo juu (au andiko ambalo wewe na mkufunzi wako mtakubaliana ambalo huenda halipo kwenye orodha), tunatumai kwamba utaweza kuonyesha jinsi kifungu hiki kinavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu kwa hali yetu ya kiroho na kwa maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia tunatamani kwamba Roho akupe utambuzi wa jinsi unavyoweza kuhusianisha maana ya kifungu husika moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi wako, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika maudhui yake. Katika kila kipindi
Kukariri Maandiko
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker