Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
184 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
utahitajika kukariri na kunukuu (kwa kutamka au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. a. Luka 11:20-23
b. Mathayo 3:16-17 c. Waebrania 2:14-17 d. Warumi 8:15-17
Kila fungu la mtaala wa Cornerstone limetengewa vitabu vya kiada ambavyo vinapaswa kusomwa na kujadiliwa katika kipindi chote cha kozi. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Cornerstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi. org/books ili kupata orodha ya sasa ya nyenzo na kazi za usomaji kwa ajili ya fungu hili. Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa sababu hiyo, kama takwa mojawapo muhimu la kukamilisha mtaala huu wa Cornerstone, utatakiwa kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo ambapo utaweza kuwashirikisha wengine sehemu ya maarifa ambayo umejifunza katika kozi hii. Mwishoni mwa kila fungu, Mshauri wako atakupa mtihani wa fungu husika la kozi (huruhusiwi kutumi vitabu vya kiada wala madokezo) ambao utaufanyia nyumbani. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya kile ulichojifunza katika fungu husika na jinsi kinavyoathiri jinsi unavyofikiria au kufanya huduma kwa vitendo. Mshauri wako atakupa tarehe za kuukamilisha na taarifa nyingine utakapopokea nakala ya Mtihani wa fungu husika.
Vitabu vya Kiada
Kazi ya Huduma
Mtihani wa Mwisho wa Fungu Hili
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker