Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | UFALME WA MUNGU : KUZ I ND I L IWA KWA UTAWALA WA MUNGU / 185
Ufalme wa Mungu Kuzindiliwa kwa Utawala wa Mungu
S OMO L A 1
Ukurasa wa 105 1
Karibu katika jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya nyenzo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuonyesha kwa kutumia Maandiko kwamba tangu Anguko, utawala wa Mungu umezinduliwa katika ulimwengu huu wa sasa. • Kuelezea jinsi Yesu wa Nazareti ulimwenguni anawakilisha uwepo wa Ufalme uliodhihirishwa katika umwilisho (kuvaa mwili), kifo, ufufuo, na kupaa kwake. • Kukariri kifungu kinachohusiana na kuzinduliwa kwa utawala wa Mungu. Umesikia Tangazo? Soma Marko 1:14-15. Sote tunapenda kusikia mambo yakitangazwa. Tunapenda kusikia habari njema, hasa inapohusu kupata zawadi, kupokea baraka, kupata kitu ambacho umekitamani sana. Yesu aliposema maneno haya katika Marko, alikuwa ametoka tu kuanza kutangaza Habari Njema. Baada ya kubatizwa na Yohana Mbatizaji na kustahimili majaribu ya shetani nyikani, Yesu anaenda Galilaya. Marko anatupa makisio ya wakati kwa maneno haya: Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani. Kwa hiyo, ilikuwa ni mapema katika huduma ya Yesu, muda baada ya tangazo ambalo Yohana Mbatizaji alikuwa amelitoa kuhusu Yesu kuma Mpakwa-Mafuta ajaye. Yesu, katika wakati huu muhimu katika historia ya wokovu anakuja akitangaza, na kuzindua kiuhalisia (kuanza rasmi) mahubiri na huduma yake ya Ufalme. Yesu alitambua umuhimu wa wakati huo, akidokeza kwamba “wakati umetimia,” yaani, wakati ulionenwa na manabii kwamba utawala wa Mungu ulikuwa umefika. Bila mbwembwe, bila tarumbeta, fataki, au makusanyiko makubwa na misafara ya waheshimiwa, Mesihi anatangaza kwamba Ufalme umekuja, yaani, kwamba ulikuwa “umekaribia.” Utawala wa Mungu, ambao ulikuwa umeahidiwa na kutamaniwa, ulikuwa umefika sasa kwa kuja kwa Yesu wa Nazareti ulimwenguni. Pamoja na kuvutia na ukuu wa tangazo hili, ni wachache sana waliolisikia na kulielewa katika uzito na uhalisia wake – kuanzishwa kwa utawala wa Mungu, mwisho wa uasi wa shetani, mwisho wa laana, na ahadi ya maisha mapya katika Ufalme wa Mungu. Ni wachache tu waliouelewa
Malengo ya Somo
1
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Ibada Ukurasa wa 105 2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker