Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
186 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
ujumbe ule siku hiyo. Vipi leo? Je, unamsikia Mwana wa Mungu akitangaza leo kwamba “Ufalme wa Mungu umekaribia?” Ushauri wake ni wenye kutoa uhai na wa ajabu leo kama ilivyokuwa siku ile kwa watu wa kawaida huko Galilaya; tukimsikia akisema sasa, leo, tunaweza kumrudia Mungu, kugeuka kutoka katika dhambi, na kukumbatia ukweli wa Habari Njema katika Kristo. Tunaweza kuja chini ya utawala wa Mungu ikiwa tu tutaitikia tangazo hili, na kuitikia sauti ya Mwokozi leo.
Baada ya kutamka na/au kuimba ukiri huu wa imani (taz. Kiambatisho) omba maombi yafuatayo:
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Mungu Mwenyezi, kwa kifo cha Mwanao umeiharibu dhambi na mauti, na kwa ufufuo wake umeleta haki, yaani kutokuwa na hatia, na uzima wa milele, ili sisi, tukiwa tumekombolewa kutoka katika nguvu za ibilisi, tukae katika Ufalme wako. Utujalie tuyaamini haya kwa moyo wote na, tukiwa thabiti katika imani, kukusifu na kukushukuru; kwa njia ya Mwanao Yesu Kristo Bwana wetu, Amina. ~ Martin Luther amenukuliwa na Andrew Kosten. Ibada na Maombi ya Martin Luther . Grand Rapids: Baker Book House, 1965. uk. 49.
1
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita, yaani Yohana 15:18-20.
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukabidhi
KUJENGA DARAJA
Ungejibuje Swali Lifuatalo? ”Mungu alianza kuzindua (yaani, kuanza) utawala wa ufalme wake maishani mwangu wakati …….” Je, unaweza kubainisha wakati ambapo Mungu alianza kazi ya ufalme wake katika maisha yako? Je, aliianza siku ulipotubu na kuamini? Siku ambayo ulikuja kuwa mshiriki wa kanisa lako la mahali pamoja? Siku ulipozaliwa kimwili, au kabla ya hapo? Ikiwa ungekisia tarehe ambayo kazi ya ufalme wa Mungu ilianza katika maisha yako, ungesema ni lini?
1
Ukurasa wa 106 3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker