Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | UFALME WA MUNGU : KUZ I ND I L IWA KWA UTAWALA WA MUNGU / 187
Kweli au Si kweli? ”Ni vyema kusema kwamba Ufalme wa Mungu haujawahi kuwa na mwanzo au uzinduzi wowote, kwa kuwa Mungu amekuwa Mungu siku zote, na kama Mungu, amekuwa akitawala siku zote.” Je, kipi ni sahihi kuhusu kauli hii? Je, kuna chochote hapa ambacho kinaweza kupotosha? Je, utawala wa Mungu katika maisha ya mtu, familia, au taifa una mwanzo, au je, Mungu amekuwa Bwana wa maisha yetu daima, bila kujalishwa kwamba tunakiri hivyo au la? Utashi Katika historia yote ya falsafa na theolojia, watu wacha Mungu, wanyoofu wamejadiliana juu ya swali la uhuru wa kuchagua, yaani, je, kweli tuna kitu chochote kama hiari ndani yetu? Fikiria juu ya hilo kwa muda. Ikiwa ungeulizwa, “Je, tuko huru?”, ungesema nini? Sisi kama wanadamu tuko huru kufanya nini? Je, sisi ni watumwa wa dhambi, au watumwa wa Mungu, au tuna chaguo katika kila jambo tunalolifikiria, tunalofanya na tunalokutana nalo? Ikiwa hatuna uhuru wa kuchagua, Mungu anawezaje kutuwajibisha kwa yale tunayosema na kufanya? Mungu amekuwa akifanya kazi tangu mwanzo ili kukomesha kutotii na uasi wote ambavyo ni matokeo ya Anguko, kupitia kufunuliwa kwa ahadi yake ya agano kwa Ibrahimu ya kuleta Mzao. Ahadi hii inaweza kufuatiliwa kupitia watu wa Mungu wa agano, kupitia Yuda, Daudi. Ijapokuwa watu wa Mungu walishindwa kiadili na kuabudu sanamu, kupitia kwao alitokea Mtiwa-Mafuta, Yesu wa Nazareti, anayewakilisha kutimizwa kwa ujio wa Ufalme. Kwa uwezo na mamlaka ya mwisho, utawala wa Mungu umedhihirishwa kupitia kuvaa mwili kwa Yesu, kifo, ufufuo, na kupaa kwake. Lengo letu la somo hili la Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Katika nafsi na kazi za Yesu wa Nazareti, Utawala wa ufalme wa Mungu umezinduliwa kwa utukufu (katika maana ya mwisho), na kutimizwa ulimwenguni. • Yesu alitoa ushahidi na uzima kwa utawala wa Mungu kama Christus Victum kwa njia ya mateso, kifo, na kuzikwa kwake. Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu Mch. Dr. Don L. Davis
2
3
1
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
MAUDHUI
Muhtasari Ukurasa wa 106 4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker