Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
20 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. (Ona Kiambatisho husika kupata Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko. Mkufunzi wako atakupatia fomu hii)* Tafadhali, ona Utangulizi wa kifa fungu kupata Maandiko mahususi ya Kukariri kwa fungu husika. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, eksejesia au ufafanuzi wa Maandiko) kwa kila kifungu . Kazi yako iwe na kurasa tano ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono, na iweze kushughulikia mojawapo ya vipengele mbalimbali vya nafsi na kazi ya Mungu Baba vilivyoangaziwa katika kozi hii. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko kuleta badiliko na athari chanya katika maisha yako na ya wale unaowahudumia. Unapoendelea kujifunza kozi hii, uwe huru kuongeza mistari kadhaa katika uchambuzi wako (takriban mistari 4-9) kuhusu jambo ambalo ungependa kujifunza kwa kina. Maelezo ya kazi hii yanapatikana kwenye ukurasa wa 23, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi cha kozi hii. Pia tazama Utangulizi wa kila fungu kwa maelekezo zaidi kuhusu Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya kazi hii yanapatikana kwenye ukurasa wa 25, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi cha kozi hii. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako.
Kukariri Mistari ya Biblia
Kazi za Ufafanuzi wa Maandiko
Kazi za Huduma
Kazi za Darasani na za Nyumbani
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker