Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

MUHTASAR I / 21

Kila fungu katika mtaala wa Cornerstone limeainisha vitabu vya kiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza kozi hiyo. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya mtaala wa Cornerstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumientree.com ili kupata orodha ya sasa ya vitabu vya kiada na vitabu vya rejea vinavyohitajika kwa ajili ya fungu hili mahususi la kozi hii. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. (Angalia Kiambatisho husika kupata Fomu ya Ripoti ya Usomaji. Mkufunzi wako atakupatia fomu hii).* Mwishoni mwa kila fungu, Mshauri wako atakupa mtihani wa fungu husika la kozi (huruhusiwi kutumi vitabu vya kiada wala madokezo) ambao utaufanyia nyumbani. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya kile ulichojifunza katika fungu husika na jinsi kinavyoathiri jinsi unavyofikiria au kufanya huduma kwa vitendo. Mshauri wako atakupa tarehe za kuukamilisha na taarifa nyingine utakapopokea nakala ya Mtihani wa fungu husika. Fomu ya Kukagua Kazi inapatikana katika Viambatisho. Gredi za ufaulu Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi. A – Kazi Bora D – Inaridhisha (Wastani) B – Nzuri Sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako

Kazi za Usomaji

Mtihani wa Mwisho wa kila Fungu

Fomu ya Kukagua Kazi

* Washauri wanaweza kupakua Orodha ya Kukagua Kazi, Fomu ya Kusahihisha Ukariri wa Maandiko, na Fomu ya Ripoti ya Usomaji kutoka kwenye Dashibodi ya WIU.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker