Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
22 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote.
Masharti ya Cheti cha Cornerstone Ili kupata Cheti cha Cornerstone, mwanafunzi lazima atimize masharti yafuatayo: • Kukamilisha mahitaji yote ya kozi kwa kila fungu la Mtaala wa Cornerstone na kupata ufaulu wa angalau 70% katika kila fungu. • Kukamilisha kozi ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini . Credit kwa ajili ya Cheti cha TUMI Mwanafunzi analiyekamilisha masomo ya ngazi ya Cheti ya Cornerstone anaweza kuendelea na masomo yake ya TUMI na kufanyia kazi mojawapo ya kozi zetu za ngazi ya cheti zenye credit hours 32. Kazi iliyofanywa kwa ajili ya cheti cha Cornerstone itamnufaisha mwanafunzi huyo kwa njia zifuatazo: • Cheti cha Mafunzo ya Kitheolojia ya Mijini (yaani, Certificate in Urban Theological Studies, kwa ufupi CUTS) - Cheti cha Cornerstone kitahesabiwa kama credit hours 6 kuelekea CUTS. • Cheti katika Mafunzo ya Uongozi wa Kikristo ( Christian Leadership Studies , CLS) - CLS ni cheti kinachotunukiwa wale wanaokamilisha moduli zote 16 za Capstone. Cheti cha Cornerstone kitahesabiwa kama credit hours 6, au sawa na moduli 3, kuelekea CLS. Mwanafunzi anaweza kutimiza muda wa mafunzo uliosalia kwa kukamilisha moduli 13 zozote atakazochagua kutoka katika mtaala wa Capstone.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker