Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
MUHTASAR I / 23
Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko Kama sehemu ya ushiriki wako katika Mtaala wa Cornerstone, kwa kila fungu la kozi hii utahitajika kufanya ufafanuzi, yaani eksejesia (uchambuzi wa ndani wa andiko) juu ya kifungu fulani cha Neno la Mungu. Kusudi la kazi hii huu ya ufafanuzi wa Maandiko ni kukupa fursa ya kufanya uchambuzi wa kina wa kifungu muhimu kuhusu asili na kazi ya Neno la Mungu. Unapojifunza mojawapo ya vifungu vya Maandiko yaliyoorodheshwa chini ya “Kazi za Fungu la Kozi” mwanzoni mwa kila Sehemu, tunatumaini kwamba utaweza kuonyesha jinsi andiko hicho kinavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu kwa ajili ya hali yetu ya kiroho na kwa ajili ya maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia tunatamani kwamba Roho akupe ufahamu kuhusu jinsi unavyoweza kuhusianisha maana yake moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia , ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika ? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo ? 3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu ? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa . Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika).
Dhumuni
Mpangilio na Muundo
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker