Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
212 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
II. Nadharia za Utatu Kutokana na Historia
A. Nadharia ya oikonomia (yaani Mgawanyo wa Majukumu): nafsi tatu zinahusika katika viwango mbalimbali katika uumbji na ukombozi.
1. Hippolytus na Tertullian (mababa wa awali wa Kanisa)
2. Mtazamo huu haukufanya jaribio la kuchunguza mahusiano baina ya washiriki watatu wa Utatu.
3. Ulizingatia uumbaji na ukombozi: Mwana na Roho sio Baba, lakini wameungamanishwa na Mungu katika asili yake ya milele.
2
B. Nadharia ya Mungu Mmoja Mwenye Nafsi Moja (“ Dynamic Monarchianism ”): Mungu alikuja kwa nguvu juu ya nafsi ya Yesu.
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
1. Ilianzishwa kipindi cha mwishoni mwa karne ya 2 na karne 3 na Theodotus
2. Mungu alikuwepo katika maisha ya mtu huyo, Yesu wa Nazareti.
a. Mungu alikuwa nguvu inayofanya kazi juu, ndani, au kupitia Yesu, lakini hakuwa na uwepo halisi ndani ya Yesu.
b. Kabla ya ubatizo wake, Yesu alikuwa mtu wa kawaida tu (ingawa alikuwa mwadilifu sana), rej. Mt. 3:16-17.
c. Wakati wa ubatizo, Roho alishuka juu ya Yesu, na nguvu za Mungu zilitiririka kupitia kwake kuanzia hapo na kuendelea.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker