Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | MUNGU BABA : MUNGU KAT I KA UTATU – UKUU WA MUNGU / 215
Hitimisho • Neno la Mungu linafundisha kwamba kuna Mungu mmoja tu, na kwambaMungu huyo anajifunua kwetu kama Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. • Zaidi ya hayo, Maandiko hayafundishi tu kwamba Mungu ni Mungu mmoja, bali pia yanamzungumzia Mungu katika nafsi tatu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yameibuka kutokana na video. Fundisho la Biblia juu ya Utatu si rahisi wala jepesi kuelewa. Kinachopaswa kueleweka, hata hivyo, ni kwamba Utatu ni jaribio la kukubali kwa mamlaka na uaminifu wote ushuhuda wa kimaandiko kuhusu umoja wa Mungu kama Mungu mmoja, na wakati huo pia kukubali uungu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Fanya mapitio ya dhana kuu kuhusu fundisho hili muhimu, na uhakikishe kwamba unaouwezo wa kutetea madai yoyote unayotoa kwa kutumia Maandiko yenyewe (Mdo 17:11). 1. Nini maana ya “fundisho la Utatu ?” Neno hili linarejelea fundsho lipi la Biblia? 2. Fanya muhtasari wa namna Maandiko yanavyosisitiza kwamba Mungu ni mmoja, wakati huo huo, yakiuthibitisha uungu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. 3. Toa mifano ya baadhi ya uthibitisho wa kibiblia unaothibitisha kwamba kila mshiriki wa Utatu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) ni Mungu, (yaani, tumia Biblia kuonyesha jinsi kila mshiriki wa Utatu alivyo na sifa za Mungu, anavofanya kazi ya Mungu, anavyoitwa Mungu, na kutumia mamlaka kama Mungu). 4. Ni kwa namna gani tunaweza kuthibitisha umoja wa Mungu, na wingi wa Mungu? 5. Nini maana na uhusiano wa nafsi za Mungu na kiini kimoja cha Mungu? Kanisa limejaribu kwa namna gani kuelewa mafundisho ya Biblia kuhusu Utatu? (toa mfano). 6. Kwa nini ni lazima kabisa kutosema kamwe kuwa wazo la Utatu linamaanisha miungu watatu? Kwa nini kanisa limekuwa makini sana kutofautisha Uungu mmoja wa Mungu huku likithibitisha nafsi tatu za Mungu ? 7. Kanuni za Imani hutusaidiaje kuelewa jinsi jambo fulani lisivyo la kweli kuhusu Utatu? Je, Unaweza kukataa wazo lolote kati ya haya – umoja wa Mungu, utofauti kati ya Baba,
Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu Ukurasa wa 117 4
2
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker