Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
216 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Mwana, na Roho Mtakatifu, na usawa wa washiriki wote wa Utatu – na bado ukawa na mtazamo wa Utatu unaokubalika?
UHUSIANISHAJI
Somo hili linajikita katika asili ya Utatu Mtakatifu na sifa za ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi. Fundisho la Utatu linathibitisha madai ya Maandiko kwamba Mungu ni mmoja na bado yuko katika nafsi tatu tofauti, ambazo zote zinarejelewa kama Mungu, na zinashiriki utukufu wa asili ya uungu. Mungu Baba, nafsi ya kwanza ya Utatu, anazo sifa zinazozungumza kwa nguvu na kwa uhakika kuhusu ukuu wake. Kama Mungu Baba alivyo roho, anao uzima ndani yake, haiba yake ni halisi, hana ukomo katika asili na tabia yake ya kiungu, na ana uhalisia usio badilika. • Fundisho la Utatu linarejelea fundisho la Biblia kuhusu utatu wa Mungu. • Maandiko yanasisitiza kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine isipokuwa Mungu mmoja, na bado yanasisitiza kwamba Mungu huyu mmoja amejifunua kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. • Kila mshiriki wa Utatu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) anazo sifa za Mungu, anafanya kazi ya Mungu, anaitwa Mungu, na hutumia mamlaka kama Mungu. • Biblia inathibitisha umoja wa Mungu, na wingi wa Mungu (kwamba Uungu ni zaidi ya nafsi moja), na nafsi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu zinatajwa kwa pamoja kama nafsi katika Ukamilifu wa Uungu Mtakatifu. • Fundishola Utatu linasisitiza kwamba Mungu yuko katika nafsi tatu, na kwamba washiriki wote wa utatu wanashiriki asili moja, wanatofautiana katika haiba na kazi zao, na bado wanalingana katika utukufu, kwa pamoja wakimkamilisha Mungu mmoja wa kweli, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafuzi wenzako maswali magumu uliyonayo kuhusu Utatu na sifa za kiungu za ukuu wa Baba. Bila shaka unayo maswali kadha wa kadha ambayo yamekuja akilini ulipokuwa ukisikiliza, ukijifunza, ukiomba, na kutafakari mada hizi kuu za Neno la Mungu. Chukua muda, kukusanya maswali yako mwenyewe kuhusu mada hizi na nyingine zinazofanana nazo, na uwashirikishe wanafunzi wenzako. Shirikianeni kwa pamoja juu ya mambo yaliyojitokeza katika kusoma kwenu somo hili. Pengine maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kuwaongoza katika mielekeo tofauti.
Muhtasari wa Dhana Muhimu
2
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker