Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | MUNGU BABA : MUNGU KAT I KA UTATU – UKUU WA MUNGU / 217

• Je, mtu anaweza kuwa Mkristo na bado akalikataa fundisho la Utatu ? Ni fundisho la muhimu kama lile la wokovu kwa neema kwa njia ya imani, au mtu anaweza kuwa na mtazamo tofauti juu ya Mungu na bado akachukuliwa kuwa mwamini wa kweli? • Kwa kuwa neno “Utatu” lenyewe halipo katika Biblia, theolojia inawezaje kulifanya kuwa “fundisho muhimu” la imani? • Je, mtu anaweza kuamini jambo fulani kuhusu Mungu kama vile Mashahidi wa Yehova wanavyoamini (Mungu Baba pekee ndiye Mungu; Yesu ni wa pili kwa ukuu na ameumbwa na Mungu, na Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu kwa ajili ya huduma) na bado akachukuliwa kuwa sawa kibiblia? Ikiwa ndiyo, kwa nini? Kama siyo, kwa nini? • Unawezaje kuuelewa sana ukuu wa Mungu kiasi cha kuathiri kila ufanyalo: ibada, mwenendo na tabia, na huduma yako? Unawezaje kuufanya ukweli huu mkuu kuwa maisha yenye nguvu kwa ajili ya Mungu? • Wengi humtazama Mungu kama anayetaka kukidhi mahitaji yao, na si kama Mungu katika Utatu na mkuu wa ulimwengu. Unawezaje kubadili mtazamo huu kutoka kumtazama Mungu kama aishiye kwa ajili yangu hadi kumtazama Mungu kama ambaye kwake vitu vyote vimepata kuwepo ? • Ni njia zipi zinazoweza kuwasaidia kwa vitendo waamini wanaokua kutamani na kujifunza “kweli za ndani zaidi” za Neno la Mungu kuhusu sifa, tabia, na jina la Mungu? • Sifa za ukuu wa Mungu (yaani, hali yake ya kiroho, uzima, nafsi, kutokoma, na kudumu kwake) zinaonyesha jinsi Yeye alivyo juu kabisa ya ufahamu wetu. • Je, ni kwa jinsi gani imani yetu katika Yesu Kristo inatufanya tuweze kumfikia Baba zaidi? (rej. Yoh. 1:18; Yoh. 14:7-9) ”Haileti Maana Yoyote” Wakati wa mfululizo wa somo la sifa za Mungu katika mafundisho ya Biblia ya Mchungaji katikati ya juma, mwamini mchanga mwenye njaa, anainua mkono wake na kutoa maoni kuhusu somo hilo. “Mchungaji,” anasema kama mwenye kutoa utetezi, “Ninajua kwamba hii inaweza kuwa muhimu katika mazingira ya seminari, lakini kiukweli, ninapata shida kuona kwa nini tunapaswa kujifunza maneno na vitu vyote hivi vinavyochekesha kuhusu Mungu. Tuna haja gani ya kuelewa yale ambayo Wakristo waliyaamini zamani kabisa huko kuhusu asili ya Mungu, au kutumia maneno mengine

2

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

MIFANOHALISI

1

Ukurasa wa 118  5

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker