Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

218 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

kama ousios or homousia au maneno yoyote magumu ya aina hiyo. Nataka tu kujua habari za Yesu, kwa kweli sijali sana kuhusu fundisho hata hivyo. Je unaweza kuniambia ni kwa nini, mimi kama mwamini mchanga, natakiwa kupendezwa na mambo yote haya, kwangu hayaonekani kuwa muhimu sana, wala hayaonekani kuendana na jambo lolote ninalofanya.” Kama mchungaji, ungejibuje swali hili linaloulizwa na dada huyu mpendwa katika Kristo? Mungu Mmoja, katika Namna Tatu Mwinjilisti/mhubiri maarufu wa televisheni amejitokeza hivi karibuni na mtazamo wa utatu ambao umeleta mkanganyiko mkubwa katika jamii za Kikristo. Badala ya kuthibitisha maoni ya kimapokeo ya Kikristo kuhusu Utatu kuwa Mungu ni mmoja anayejidhihirisha katika nafsi tatu tofauti (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu), mwalimu huyo maarufu anaamini kwamba kuna Mungu mmoja ambaye kwa hujidhihirisha katika namna tatu kutegemeana na hali na mazingira. Kwa maneno mengine, wakati anathibitisha kwamba Mungu ni mmoja, anapinga utofauti wa nafsi za Utatu. Kuna Mungu mmoja tu anayejidhihirisha katika namna tatu tofauti. Kwa nini mtazamo huu haukubaliki kulingana na Neno la Mungu? Je, ungeutazama mtazamo huu kuwa uzushi na upotofu? Kama ndiyo, kwa nini? Ikiwa siyo, kwa nini? “Urafiki Usio na Afya” Nyimbo nyingi sana za sifa na kuabudu leo zinaangazia ukaribu na uhusiano binafsi ambao mwamini anao sasa na Mungu. Nyimbo nyingi zinamzungumzia Mungu kama rafiki, msiri, hata kama mpenzi, zikiweka msisitizo katika kina binafsi cha uhusiano wetu na Mungu. Hata hivyo, ni wazi kwamba kwa kukosekana kwa fundisho thabiti katika mengi ya makanisa yetu, na kwa kupunguza uimbaji wa nyimbo za tenzi katika mikusanyiko mingi, waamini wengi hawana ufahamu wa sifa za ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi. Katika uhalisia, Mungu wa makanisa mengi ni mkubwa kiasi cha kuweza tu kukidhi haja za mioyo yetu, si kushughulikia matatizo ya ulimwengu, achilia mbali kuukomboa ulimwengu katika hali yake ya kutoweza kudhibitiwa. Kama mtu mmoja aliyewahi kuliongelea hili alivyosema: Mungu wa makanisa mengi ni rafiki mwema, lakini haonekani kuwa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunaonekana kuwa na urafiki usio na afya na Yeye ambaye ni moto ulao.” Fikiria kwamba Bwana amekuita kuwa mhudumu wa muziki na ibada katika kanisa. Orodhesha misisitizo au vitu nane tofauti ambavyo ungefanya kuwasaidia waamini katika kanisa lako kupata

2

2

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker