Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | MUNGU BABA : MUNGU KAT I KA UTATU – UKUU WA MUNGU / 219

uelewa mkubwa, wa thamani, na wa kibiblia wa ukuu wa Mungu katika ibada na maisha kwa ujumla.

Fundisho la Utatu ni funidisho la kibiblia linalothibitisha kwamba asili ya Mungu ni umoja wa nafsi tatu zinazoshiriki kiini kimoja kama Mungu. Biblia inasisitiza kwamba Mungu ni mmoja (Kum. 6:4), na Mungu huyu mmoja yuko katika nafsi tatu tofauti lakini zenye usawa, za milele, kila moja inatajwa kama Mungu katika Maandiko, na zinashiriki utukufu wa asili ya kiungu. Utatu Mtakatifu (yaani, Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) ni jina linalotumika ili kuthibitisha kile ambacho Maandiko yenyewe yanasema juu ya umoja, utofauti, na usawa wa washiriki wa Uungu mmoja. Mungu Baba Mwenyezi, nafsi ya kwanza ya Utatu, anazo sifa zinazozungumza kwa nguvu na kwa uhakika kuhusu ukuu wake. Kama Mungu, Baba ni roho, ana uzima ndani yake, haiba yake ni halisi, hana ukomo katika asili na tabia yake ya uungu, na habadiliki katika asili yake. Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo juu ya asili ya Utatu na ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi, unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo (tahadhari: vitabu hivi vina maudhui magumu!): Charnock, Stephen. The Existence and Attributes of God . Grand Rapids: Baker Book House, 1996. O’Collins, Gerald, S. J. The Tripersonal God: Understanding and Interpreting the Trinity . Mahwah, NJ: Paulist Press, 1999. White, James R. The Forgotten Trinity: Recovering the Heart of Christian Belief . Bloomington, MN: Bethany House Publishing, 1998. Fundisho la Utatu na ukuu wa Mungu Baba sio mada tu za kitheolojia za kujifunza na kuwekwa kando. Kinyume chake, hizi ndizo kweli kuu za imani, na wale wanaozitafakari kwa muda mrefu hubadilishwa milele kutokana na kutafakari huko. Kuzihusisha kweli hizi katika maisha na huduma yako kunaweza kukabadilisha maisha na huduma yako; gharama ni utendaji makini wa Neno la Mungu kwenye maisha yako. Unapoendelea kutafakari juu ya mafundisho ya somo hili, muulize Bwana ni kwa namna gani angekutaka utajirishe, ubadilishe, na kugeuza namna yako ya kufanya huduma kupitia kweli hizi ambazo Roho mtakatifu amekuonyesha hapa. Unapozitafakari kweli hizi, na kufikiri kuhusu maisha yako mwenyewe na huduma iliyo unganishwa nazo, tafuta kutambua kile ambacho Roho anaweza kuwa anakuita kufanya sasa hivi, kama kipo, kuhusu kweli hizi. Tumia muda mbele za

Marudio ya Tasnifu ya Somo

2

Nyenzo na Bibliographia

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Kuhusianisha Somo na Huduma

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker