Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
220 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Bwana ukitafakari juu ya kweli kuhusu asili na ukuu wa Mungu, na umuulize ni jinsi gani au kwa namna gani unaweza ukafanyia kazi kikamilifu fundisho hili. Pia, unapofikiria kuandika kazi yako ya Huduma kwa Vitendo kwa ajili ya moduli hii, unaweza kuunganisha kazi yako na mada fulani hapa. Mtafute Bwana ili akupe mwelekeo wake, na urudi juma lijalo ukiwa tayari kuwashirikisha wanafunzi wengine darasani kwako kuhusu mawazo yako. Katika kutafakari kweli hizi juu ya asili ya Mungu kama Bwana wa Utatu na juu ya ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi, mtu huanza kuona utoshelevu wa Mungu wetu kukidhi kila hitaji, si tu katika maisha binafsi ya mtu lakini katika maisha ya wale tunaowapenda na kuwatumikia. Labda katika kipindi cha somo hili, wakati ukitafakari juu ya ukuu wa Baba, kuna hitaji fulani muhimu ambalo limefunuliwa kwako. Pengine Roho Mtakatifu amekufanya kuzingatia suala, hitaji, au jambo fulani, na unahitaji kumtafuta Bwana kwa ajili ya uweza na msaada wake katika jambo hilo. Sasa ni wakati wa kushirikishana mahitaji yenu na kuombeana. Kama muda hautawaruhusu kuomba pamoja sasa hivi, tafuteni watu wa kuhirikiana nao katika maombi ambao mnaweza kuwashirikisha mizigo yenu na ambao atayapeleka maombi yenu mbele za Bwana. Bila shaka, tambueni kuwa mwalimu wenu atakuwa tayari na wazi kabisa kuomba nanyi, pamoja na viongozi wenu wa kanisa, hasa mchungaji wako. Msikilize Bwana na umruhusu Roho Mtakatifu akuongoze katika kumshirikisha haja zako Baba Mwenyezi, Mungu wetu mkuu na mwenye enzi na Bwana wa wote.
Ushauri na Maombi
2
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
KAZI
Mathayo 3:16-17
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books kupata kazi ya kusoma ya juma lijalo, au muulize mkufunzi wako.
Kazi ya Usomaji
Kwa mara nyingine, hakikisha kwamba umesoma kazi zilizo hapo juu, na kama wiki iliyopita, ziandikie muhtasari mfupi na ulete muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Tafadhali ona “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” katika ukurasa wa 16). Kadhalika, sasa ndio wakati wa kuanza kufikiria kuhusu muktadha wa kazi yako ya huduma kwa vitendo, na pia kuamua ni kifungu gani cha Maandiko utakachochagua kwa ajili ya kazi yako ya ufafanuzi wa Maandiko ( eksejesia ). Usichelewe kufanya maamuzi juu ya kazi yako ya huduma
Kazi Zingine Ukurasa wa 118 6
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker