Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | MUNGU BABA : MUNGU KAT I KA UTATU – UKUU WA MUNGU / 221

na ile ya ufafanuzi wa Maandiko. Kadiri unavyofanya maamuzi mapema, ndivyo utakavyopata muda wa kutosha kujiandaa!

Katika somo letu linalofuata, Mungu Mwana: Yesu, Masihi na Bwana wa Wote – Alikufa , tutachunguza maana za kitheolojia za unyonge na kifo cha Yesu, kushuka kwake katika utu wake wa kiungu kwa niaba yetu. Tutaangazia kunyenyekezwa kwa Yesu kwa njia ya Umwilisho (incarnation) , maisha na huduma yake, pamoja na kifo chake. Katika kuzingatia dhabihu yake pale Kalvari, tutachunguza baadhi ya mifano ya kihistoria inayosaidia kuelewa kazi yake juu ya msalaba. Hii inahusisha mtazamo wa kifo chake kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho (utoshelevu wa kiungu) kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Pia tutachunguza baadhi ya maoni mbadala ya kihistoria kuhusiana na kifo cha Yesu. Haya ni pamoja na kifo chake kama 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. Huenda hakuna fundisho linaloweza kulinganishwa na msisimko unaotokana na kuelewa kwa njia ya kibiblia na ya kiimani utajiri, ajabu, na fumbo la Mwana wa Mungu, Yesu wa Nazareti. Kufedheheshwa kwake na kupaa kwake ndicho kiini cha Injili, na kitovu cha uchaji, ibada na huduma yetu. Mungu atumie somo hili kuhusu mtu wake mtukufu kukuwezesha kumpenda zaidi na kumtumikia yeye ambaye pekee ndiye aliyepewa ukuu na Baba. Tafadhali tazama nyenzo zifuatazo katika kitabu cha Theolojia katika Picha: Orodha ya A-Z ya Vielelezo, Chati, Michoro na Makala Muhimu za TUMI : • Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wana Sifa na Kazi za Kiungu Zinazofanana , ukurasa wa 12 • Utatu wa Mungu katika Umoja: Utatu , ukurasa wa 505 • Kutoa Utukufu kwa Mungu , ukurasa wa 156 • Majina ya Mwenyezi Mungu , ukurasa wa 238 • Hadithi ya Mungu: Mizizi yetu Mitakatifu , ukurasa wa 40

Kuelekea Somo Linalofuata

2

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

KWA UTAFITI ZAIDI

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker