Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
226 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
au kufa pamoja naye; Mfalme wetu aliyesulubiwa aliye hai, na anayetawala milele pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja milele na hata milele. ~ Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. Kitabu cha Mhudumu cha Kutumika Pamoja na Ekaristi Takatifu na Sala ya Asubuhi na Jioni . Braamfontein: Idara ya Uchapishaji ya Kanisa la Jimbo la Afrika Kusini. uk. 47.
Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Mathayo 3:16-17.
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za Kukusanya
3
KUJENGA DARAJA
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Msalaba Mfukoni Mwako Msalaba bila shaka ni mojawapo ya alama zinazoonekana sana za imani ya Kikristo, na ambayo kusema ukweli haieleweki sana. Leo, msalaba unawakilishwa kwa kila njia inayofikiriwa, kuanzia kwenye vishaufu, pete na vipini hadi kwenye vibweta vya mikufu, juu ya vikuku na Tisheti, na kwenye sanaa na usanifu wa kanisa. Ni bidhaa kuu katika nchi za Magharibi na inayodharauliwa katika sehemu nyingi za dunia. Kampuni moja hutengeneza msalaba wa saizi ya sarafu ambayo inafaa kubebwa mfukoni ili kukukumbusha gharama iliyolipwa kwa ajili ya dhambi zetu. Je, una maoni gani kuhusu biashara ya msalaba, na ni jinsi gani shughuli kama hizo zinaweza kutufanya tusijue maana ya kweli ya mateso ya Kristo? Mateso ya Kristo Kakitka kuitikia kwa habari ya filamu maarufu zaidi ya Mateso ya Yesu (The Passion of the Christ) , makanisa mengi ya Kiinjili yalifanya mikutano ya kiinjilisti iliyobuniwa kwa kusudi la kutangaza Habari Njema sambamba na uingizwaji wa filamu hiyo sokoni. Hali ya picha ya mateso ya Masihi iliyoonyeshwa katika filamu ile imesababisha mwitikio wa aina tofauti, kuanzia hisia za kina za
1
Ukurasa wa 123 3
2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker