Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MUNGU MWANA : YE SU, MAS I H I NA BWANA WA WOT E – AL I KUFA / 227

majuto na upendo hadi mshtuko na hofu. Filamu hiyo labda ndio taswira ya ukatili wa kutisha zaidi kuwahi kuigizwa kuhusiana na mateso ya Yesu. Wengine wamesema maonyesho kama haya yameenda mbali mno katika kuangazia ukatili wa Kalvari bila kufunua kwa kiasi kikubwa sababu za msingi za ukatili huo. Je, una maoni gani kuhusu tafsiri hizo za ajabu za mateso ya Yesu. Je, tunapaswa kutoa zaidi ya hizi, au tumezipata za kutosha kwa sasa? Kimya cha Ajabu Katika makanisa yetu mengi yanayozingatia zaidi kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya “watafutaji”, tunashuhudia ukimya wa ajabu kwa habari ya unyanyapaa na mateso ya Kalvari. Mengi ya mahubiri na homilia ni kuhusiana hasa na mada zinazovutia watu wengi, na kwa kawaida yanaepuka mada na jumbe ambazo zina mkazo mkubwa wa kitheolojia na mafundisho ya kidini. Msalaba unapozungumziwa, kwa kawaida huzungumziwa kwa namna inayomafanya msikilizaji ajisikie kuwa ana uwezo na ni wa thamani badala ya kuwa suluhisho la wazi la uasi wa wanadamu. Nafasi ya mafundisho hukusu dhabihu ya damu ya Masihi imechukuliwa na mahubiri juu ya mawazo chanya na kujenga kumbukumbu za familia. Nafasi ya nyimbo nyingi za zamani ambazo zilizungumzia ajabu, nguvu, na siri ya msalaba imechukuliwa na mafuriko ya pambio ambazo zote zinalenga furaha ya mwabudu na sio mateso ya msingi ambayo yalifanya ibada iwezekane. Ingawa makanisa mengi yanaendelea kusisitiza msalaba kama tukio kuu katika historia ya wokovu, mbinu zetu za uinjilisti na uenezaji wa Habari Njema zinalenga zaidi mada chanya kwa ajili ya kuvutia wageni wapya. Je, una maoni gani kuhusu kuongezeka kwa ukimya huu wa kustaajabisha kuhusiana na msalaba katika mahubiri, mafundisho na ibada za makanisa yetu leo?

3

3

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Yesu, Masihi na Bwana waWote: Alikufa Kunyenyekezwa na Kifo chake

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

MAUDHUI

Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, tukitumia maneno ya mwanatheolojia Oden, kunahusu kushuka kwake kutoka mbinguni akiuacha utukufu wake wa kiungu, kuja duniani na kufa kwa ajili ya ulimwengu. Unyenyekevu huu uliakisiwa katika kila nyanja ya Umwilisho wa Yesu na maisha yake duniani, tangu kuzaliwa kwake hadi maisha na huduma yake. Kilele cha kushuka na kunyenyekea huku kinadhihirishwa katika mateso na kifo chake pale Kalvari. Kifo chake kinaweza kueleweka kupitia vipengele mbalimbali vinavyotuwezesha kuelewa vizuri zaidi asili ya wokovu wetu ndani

Muhtasari

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker