Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
228 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
yake: kifo chake kilikuwa fidia kwa ajili yetu, upatanisho wa dhambi zetu, dhabihu mbadala badala yetu, ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Lengo letu katika sehemu hii, Kunyenyekezwa na Kifo chake , ni kukuwezesha kuona kwamba:: • Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo kunawakilishwa na kushuka kwake kutoka katika makao ya mbinguni katika utukufu wake kuja duniani kuteseka na kufa kwa ajili ya ulimwengu. • Yesu alidhihirisha unyenyekevu na kujishusha kwake katika kila hali ya Umwilisho wake, katika kuzaliwa kwake na katika maisha yake yote na huduma yake. • Kilele cha kushuka na kunyenyekea huku kinadhihirishwa katika mateso na kifo cha Yesu Kristo. • Kifo cha Yesu kinaweza kueleweka kupitia vipengele mbalimbali vinavyotuwezesha kuelewa mbaraka ambao mateso yake yaliutoa kwa ulimwengu. Vipengele hivi ni pamoja na dhana ya kifo cha Yesu kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya ibilisi na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. • Kanuni ya Imani ya Nikea inakiri wazi wazi kwamba Bwana wetu Yesu Kristo alikufa na akazikwa kwa ajili ya dhambi zetu. Huu ulikuwa mwisho na kilele cha kunyenyekezwa kwa Bwana wetu duniani katika kushuka kwake kutoka mbinguni, akiuacha utukufu wake wa kimbingu aliokuwa nao hapo awali. I. Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo Wafilipi 2:6-8 -. . . ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Wagalatia 4:4-5 - Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Muhtasari wa Maudhui ya Video
Kwa njia ya mti tulifanywa kuwa
wadeni kwa Mungu. Vivyo hivyo, kwa njia ya mti [msalaba], tunaweza kupata ondoleo la deni letu. ~ Irenaeus (c.
180, E/W), 1.545. DavidW. Bercot, ed. A Dictionary of Early Christian Beliefs . Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1998. uk. 184.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker