Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MUNGU MWANA : YE SU, MAS I H I NA BWANA WA WOT E – AL I KUFA / 237

d. Wakolosai 1:20

e. Warumi 8:19-23

2. Picha: uadui na uchungu kati ya pande mbili uliondolewa kwa njia ya upatanisho.

a. Isaya 52:7

b. Isaya 57:19

3. Kupitia kifo chake, Yesu analeta upatanisho na amani kati ya Mungu na uumbaji wake; anafikisha kwenye hitimisho la mwisho na la kudumu kule kutengwa kati ya Mungu na wanadamu (2 Kor. 5:18-20).

Hitimisho • Yesu Kristo katika kushuka kwake kutoka mbinguni alijinyenyekeza kwa njia ya Umwilisho na kifo chake. • Kupitia kazi yake msalabani, Yesu ameweka msingi wa imani, ibada na ushuhuda wetu kwa ulimwengu. • Kifo cha Yesu kimeeleweka kihistoria kupitia vipengele vya dhabihu ya fidia, upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, dhabihu mbadala badala yetu, ushindi juu ya namna Shetani anavyotushikilia kupitia kifo, na upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa na video. Kwa njia nyingi, unyenyekevu na kujishusha kwa Bwana wetu ni kiini na kielelezo cha maadili yetu binafsi katika Ufalme wa Mungu. Tumeitwa kuteseka pamoja naye, kubeba msalaba wetu kila siku, na kumfuata. Ni pale tu tunapopata kushiriki katika mateso yake ndipo tunaweza kukombolewa kikamilifu kama vyombo vyake vya ibada na ushuhuda. Haiwezekani kutotilia maanani umuhimu wa msalaba na tukawa na uongozi wa kiroho au huduma bora katika maeneo ya mijini. Jibu maswali yafuatayo kwa dhumuni la kutumia kweli hizi namna Roho atakavyo kuongoza.

3

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu Ukurasa wa 124  4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker