Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
238 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Jibu kwa uwazi na kwa ufupi na ujenge hoja zako kwa uthibitisho wa maandiko. 1. Nini maana ya kishazi “Yesu Kristo kujifanya kuwa hana utukufu?” Kwa maneno mengine, Yesu “alijiondoa” nini hasa katika Umwilisho na huduma yake duniani? 2. Maisha na huduma ya Yesu vilionyeshaje utumishi wake, unyenyekevu, na kujishusha kwake? Je, hili lina maaana gani katika maisha yetu wenyewe, ufuasi na huduma zetu leo? 3. Kuna uhusiano gani kati ya Yesu kujinyenyekeza na yeye kuacha “matumizi huru” ya sifa zake za kiungu alipokuwa duniani? 4. Kwa nini kifo cha Yesu ni muhimu sana kwa ufahamu wa jumla wa dhana ya Umwilisho? 5. Tunapaswa kuwa na uelewa gani kuhusu kifo cha Yesu kama dhabihu ya fidia kwa ajili ya ulimwengu? Elezea jibu lako. 6. Nini maana ya ukweli kwamba kifo cha Yesu ni upatanisho wa dhambi zetu? 7. Ni kwa njia gani kifo cha Yesu kwetu kina maana ya Pasaka na dhabihu mbadala? 8. Je, mzozo na mapambano kati ya kifo cha Yesu na shetani vinaonyesha sifa gani? Kwa maneno mengine, kifo cha Yesu kiliharibu kazi ya shetani kwa njia gani? 9. Kifo cha Yesu kimeletaje upatanisho kati ya Mungu na uumbaji wake na wanadamu, ukizingatia uumbaji na mwanadamu wameathiriwa sana na dhambi na laana? Somo hili linalenga juu ya kunyekezwa kwa Yesu Kristo kupitia Umwilisho na huduma, na katika maana ya kifo cha Yesu Kristo kama inavyohusiana na wokovu na ukombozi wetu. Kwa njia fulani, kweli zinazohusishwa na mada hizi ni nyenzo katika mikono ya Mungu kwa ajili ya Ufalme wake. Nyuzi zote za ufunuo wa Mungu juu yake mwenyewe kama Muumba na Mkombozi zimeungamanishwa na utu wa Yesu wa Nazareti, maisha yake makamilifu na kifo chake msalabani kama fidia mbadala. Wajibu wetu kama viongozi wa Kikristo juu ya mambo haya uko wazi kabisa: hatupaswi tu kuelewa kweli hizi katika mtazamo wa kibiblia na wa kihistoria, lazima pia tuzitafakari na kuziweka katika vitendo katika maisha na huduma zetu. Tunapaswa kufa, kama Yeye, na tunapaswa kuteseka, kama vile Bwana wetu alivyoteseka kwa ajili
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
KUJENGA DARAJA
Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker