Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | MUNGU MWANA : YE SU, MAS I H I NA BWANA WA WOT E – AL I KUFA / 239

yetu. Zingatia kwa uangalifu maana hizi unapopitia dhana kuu za somo hili zilizopo hapa chini. • Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, tukitumia maneno ya mwanatheolojia Oden, kunahusu kushuka kwake kutoka mbinguni katika utukufu wake wa kiungu, kuja duniani na kufa kwa ajili ya ulimwengu. • Unyenyekevu huu uliakisiwa katika kila nyanja ya Umwilisho wa Yesu na maisha yake ya duniani, tangu kuzaliwa kwake hadi maisha na huduma yake. Kilele cha kujishusha na kunyenyekezwa huu kinadhihirishwa katika mateso na kifo chake pale Kalvari. • Kifo cha Yesu kinaweza kutafsiriwa kupitia vipengele mbalimbali vinavyotuwezesha kuelewa mbaraka ambao mateso yake yaliutoa kwa ulimwengu. Vipengele hivi ni pamoja na dhana ya kifo cha Yesu kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya ibilisi na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Sasa ni wakati wa kujadiliana pamoja na wanafunzi wenzako maswali uliyo nayo kuhusu kunyenyekezwa kwa Yesu na kilele cha unyenyekevu na kujishusha huko kupitia kifo chake msalabani. Kama ilivyotajwa hapo juu, bila shaka ni moja ya mada muhimu zaidi ambayo sisi kama viongozi wa kiroho tunahitaji kutia juhudu kuielewa. Kuelewa maana ya kifo cha Yesu ndio moyo wa maungamo yetu na msukumo wa huduma yetu ya Kikristo. Bila shaka, maswali fulani yamekuja akilini mlipojadili na kusoma mawazo haya. Ni masuala gani hasa ambayo yamefunuliwa katika kujifunza kwako kuhusu kifo cha Kristo hadi sasa? Maswali yaliyopo hapa chini yametolewa ili kuibua maswali yako mwenyewe kuhusu kifo cha Yesu, yanayoendana zaidi na muktadha wako. • Je, kitendo cha Yesu Kristo kujifanya kuwa hana utukufu kinapaswa kuathiri vipi mitazamo yetu kuhusu maisha na huduma zetu tunapoitikia wito wa Mungu maishani mwetu? • Unyenyekevu na kujishusha kwa Yesu ni kielelezo kwetu kwa kadiri gani, na kujitiisha kwake kwa Baba ni tendo linalompasa yeye peke yake ? Elezea jibu lako. • Je, kwa sasa unatumiaje maagizo ya Yesu yafuatayo katika maisha na huduma yako? Luka 9:23-25 – “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. 24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. 25 Kwa

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi

3

Ukurasa wa 124  5

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker