Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
240 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?” • Ni kwa njia gani tunapaswa kujumuisha maandiko kama Wafilipi 2:5-11 na 2 Wakorintho 8:9 katika ufahamu wetu wa ufuasi wa Kikristo na huduma? • Kati ya picha zote zinazotolewa kuhusu kifo cha Yesu na maana yake katika maisha yetu, ni ipi ambayo wewe binafsi unaiona kuwa yenye nguvu zaidi kwa habari ya maisha na huduma yako? • Malizia sentensi ifuatayo: “Jambo moja ambalo bado linanitatiza kuhusu jinsi ninavyoelewa kifo cha Yesu ambalo nahitaji kujifunza zaidi ni ___________________________.” • Ni njia zipi ambazo utatafuta kufanya kifo cha Yesu kuwa halisi zaidi katika maisha na huduma yako? Kwa nini Meza ya Bwana ni tendo muhimu sana linaloendelea kutusaidia kufahamu maana ya mateso na kifo chake kwa niaba yetu? • Tunawezaje kufundisha vizuri zaidi unyenyekevu na kifo cha Yesu katika kuwafuasa wanafunzi wetu, kuhubiri, na kufundisha? Jadilini kwa pamoja njia mnazoweza kusisitiza tena mateso ya Kristo katika maisha ya makanisa yenu. Imani Isiyo na Damu? Mahubiri mengi ya kisasa ya Injili yanaelekea kuwekea mkazo zaidi juu ya maadili ya imani ya Kikristo , yaani, juu ya tabia ya mahusiano na maadili yanaohusishwa na imani ya Kikristo na si juu ya mateso ya Kristo, unyenyekevu wake, maumivu yake, na kifo chake Kalvari. Makanisa mengi makubwa yanayohusishwa na mbinu za ukuaji wa Kanisa na mbinu za kisasa zaidi za ibada na ushuhudiaji yako wazi katika msisitizo wao wa kwamba kushughulika kila mara na mada za ukatili na mateso, mada za kifo na dhabihu, hakuleti ufanisi katika kuwavuna wengine. Makanisa yanayokua ni yale yanayoshughulika na masuala “halisi”, yanashughulikia mahangaiko na matatizo halisi ya watu, na kuzingatia ubora wa masuala ya maisha ambayo watu wengi wa Magharibi wanahangaikia siku hadi siku. Wanabainisha kwamba mchakato wa kuingia kwenye maisha yao hauwezi kuanza na mafundisho magumu juu ya damu ya Kristo iliyomwagika, badala yake, tunapaswa kuanza na masuala ya msingi zaidi kama kazi, familia, na maendeleo binafsi. Ni wakati gani tunapaswa kuwafundisha “watafutaji” wa kweli wa Mungu mafundisho yanayohusiana na msalaba wa Kristo? Je, mafundisho hayo yanafaa kutumia kujengea “msingi” au ni ya “kupaulia” kazi ya ushuhudiaji? Elezea jibu lako.
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
MIFANOHALISI
1
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker