Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 3 | MUNGU MWANA : YE SU, MAS I H I NA BWANA WA WOT E – AL I KUFA / 241
Nadharia Zisizosahihi Kisiasa Katika ulimwengu ambao umegawanyika kwa mizozo ya kisiasa, wahubiri wengi wa kiinjili wameazimia kutotumia mifano ya kijeshi ya Agano Jipya katika kueneza imani. Ingawa sehemu kubwa ya lugha ya Yesu na mitume imetumia mifano ya kijeshi ili kuleta maana ya maisha na utume wa Yesu, ikiwa ni pamoja na kifo chake msalabani, ni walimu wachache sana ambao wanajitahidi kufuata mfano wao leo. Baadhi wameenda mbali na kudai kwamba kutumia lugha za picha kama hizi kuelezea asili ya imani ya Kikristo litakuwa kosa kubwa wakati kama huu, ambapo ubaguzi wa kidini, jihadi , vurugu na kutovumiliana vinafanyika kwa jina la miungu na dini. Taswira ya vita ni ukweli wa kutisha, na ambao hatupaswi kutumia bila tahadhari ya kweli. Wengine wanasema kwamba mifano hii imevuviwa na Mungu na imetolewa ili kutuwezesha kuelewa maana ya msingi ya ukombozi katika Kristo . Kwa maneno mengine, mifano ya vita ilichaguliwa kwa sababu inawasilisha asili ya kweli ya kiroho vizuri zaidi kuliko njia nyingine yoyote; Yesu alikuja ili kuziharibu kazi za shetani (1 Yohana 3:8). Ulimwengu uko vitani, na hakuna kiasi cha kukerwa kitakachobadilisha ukweli huu. Je, kutumia taswira ya vita katika nadharia ya upatanisho ni sahihi kwetu leo? Ufufuo, Sio Mateso! Ni wazi kwamba Agano Jipya linazingatia asili ya ufufuo kama fundisho kuu la imani ya Kikristo. Wakorintho wa Kwanza sura ya kumi na tano ni Magna Carta (Hati Kuu) ya fundisho la Kikristo: pasipo ufufuo Ukristo ungekuwa ushuhuda wa bure na wa uongo ambao haubadilishi chochote kimwili au kiroho kwa wale waliodanganyika vya kutosha kuukubali. Wengine wamedai kwamba mkazo wetu unapaswa kuwa juu ya ushindi wa ufufuo na ushindi wa kazi ya Bwana wetu, badala ya kifo cha Yesu na udhalilishaji na jeuri iliyoambatana nacho. Watu hao wanadai kwamba tukio muhimu zaidi la ushuhuda wa Kikristo ni Pasaka , sio Ijumaa Kuu , na wanadai zaidi kwamba ukereketwa juu ya kifo na jeuri ya Kalvari hausaidii kiroho wala hauna afya kisaikolojia. Ni wazi, hata hivyo, kwamba mitume waliwapa changamoto waamini wa Kanisa la kwanza kuiga mitazamo na mwenendo wao kwa kufuata kielelezo cha mateso ya Kristo na kifo chake (k.m., Flp. 2:5-11; 1 Pet. 2:21 na kuendelea; Gal. 2:20). Hata hivyo, wengi wa wale wanaopinga mkazo juu ya mateso na kifo huelekea kujikita katika kusaka utele, ustawi, afya, na utajiri wa maisha ya Kikristo badala ya ushirika wa mateso yake ili kufananishwa naye katika kifo chake (Flp. 3:10). Kuna uhusiano gani kati ya kusisitiza ufufuo wa Bwana wetu na mateso yake katika suala zima la uenezaji wa kweli wa imani ya Kikristo?
2
3
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker