Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
242 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, tukitumia maneno ya mwanatheolojia Oden, kunahusu kushuka kwake kutoka mbinguni akiuacha utukufu wake wa kiungu, kuja duniani na kufa kwa ajili ya ulimwengu. Unyenyekevu huu uliakisiwa katika kila nyanja ya Umwilisho wa Yesu na maisha yake duniani, tangu kuzaliwa kwake hadi maisha na huduma yake. Kilele cha kushuka na kunyenyekea huku kinadhihirishwa katika mateso na kifo chake pale Kalvari. Kifo chake kinaweza kueleweka kupitia vipengele mbalimbali vinavyotuwezesha kuelewa vizuri zaidi asili ya wokovu wetu ndani yake: kifo chake kilikuwa fidia kwa ajili yetu, upatanisho wa dhambi zetu, dhabihu mbadala badala yetu, ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Kifo cha Yesu kimeeleweka kwa njia mbalimbali katika historia ya Ukristo. Kila moja ya nadharia hizi za upatanisho inalenga katika mwelekeo fulani wa wokovu, na zikichukuliwa kwa pamoja zinatuwezesha kupata ufahamu mpana zaidi na uelewa wa kina wa umuhimu wa kifo cha Yesu kwa ajili yetu. Kifo cha Yesu na maana yake kimetafsiriwa kama 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. Ingawa hakuna nadharia moja kati ya hizo inayoelezea kikamilifu kifo cha Yesu, kila moja ina kweli zinazoweza kuboresha uelewa wetu wa maana na ukweli wake kwa upana mkubwa zaidi. Ikiwa utapenda kupata ufahamu wa kina zaidi kuhusu baadhi ya maarifa yaliyomo katika somo hili la Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Brown, Raymond E. The Death of the Messiah . New York: Doubleday, 1994. Kiehl, Erich H. The Passion of Our Lord . Grand Rapids: Baker Book House, 1990. Lohse, Eduard. History of the Suffering and Death of Jesus Christ . Philadelphia: Fortress Press, 1967. Stott, John. The Cross of Christ . Downers Grove, IL: InterVarsity, 1986. Unyenyekevu na kifo cha Yesu Kristo ni kitovu cha imani na utendaji wa Kikristo kiasi kwamba sisi kama viongozi lazima tuweze kuhusianisha maarifa na kweli zake na maisha na huduma zetu kila mara. Jinsi unavyoweka kweli hii katika vitendo katika maisha yako mwenyewe itaamua ufanisi wako katika kuelezea umuhimu wake katika kanisa lako na ushuhuda wako. Suala la namna ambayo Mungu angekutaka ubadilishe au uboreshe mbinu yako ya huduma
Marejeo ya Tasnifu ya Somo
3
Nyenzo na Bibliografia
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Kuhusianisha Somo na Huduma
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker