Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 3 | MUNGU MWANA : YE SU, MAS I H I NA BWANA WA WOT E – AL I KUFA / 243
kulingana na kweli hizi linategemea sana uwezo wako wa kusikia kile ambacho Roho Mtakatifu anakuambia kuhusu mahali ulipo, mahali ilipo huduma yako na uongozi wako wa kichungaji, na mahali walipo washirika wa kanisa lako. Kadhalika inategemea sana ni nini hasa Mungu anakuita kufanya sasa hivi, kuhusu kweli hizi. Panga kutumia wakati mzuri juma hili kutafakari maana ya kifo cha Kristo, na jinsi maisha yako mwenyewe yanavyohitaji kujawa na maarifa haya zaidi na kuimarishwa na kweli zilizomo. Zaidi ya hayo, unapozingatia kazi yako ya huduma katika moduli hii, unaweza kuitumia ili kuiunganisha na kweli kuhusu unyenyekevu na kifo cha Yesu kwa njia ya huduma kwa vitendo na ya moja kwa moja kwa hadhira yako, yaani yeyote utakayemchagua kumshirikisha maarifa ambayo umeyapokea. Zaidi ya yote, ni lazima tutafute kufahamu namna ambavyo Bwana mwenyewe anataka kutumia maarifa haya katika maisha yetu kuhusiana na unyenyekevu na kifo cha Kristo. Utafute uso wa Bwana wiki hii ili kupata maongozi yake, na urudi wiki ijayo tayari kuwashirikisha wanafunzi wengine wa darasa lako kile ulichokipokea kutoka kwa Bwana. Bwana anaposema nawe, ujue atakupa nafasi ya kuomba na kuombewa katika maeneo ya ukuaji ambayo ni hitaji lako leo. Labda kuna baadhi ya mahitaji maalum ambayo Roho Mtakatifu amekufunulia kupitia kujifunza kwako somo hili juu ya kifo cha Yesu. Tafuta mtu wa kushirikiana naye katika maombi ambaye anaweza kuuelewa moyo wako na mzigo ulionao, na kuungana nawe kuinua mahitaji yako mbele za Bwana. Bila shaka, mwalimu wako yuko tayari sana kutembea nawe katika hili, na viongozi wa kanisa lako, hasa mchungaji wako, bila shaka yuko katika nafasi nzuri zaidi kukusaidia kujibu maswali yoyote magumu yanayotokana na kutafakari kwako juu ya somo hili. Kuwa muwazi kwa Mungu na umruhusu akuongoze jinsi anavyotaka. Zingatia hitaji lako la kuruhusu nia ya Kristo kukaa ndani yako, na kifo cha Yesu kiwe halisi zaidi na zaidi katika kila mwelekeo wa tabia na ushuhuda wako katika Kristo.
Ushauri na Maombi
3
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
KAZI
Waebrania 2:14-17
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/ books kupata kazi ya kusoma ya juma lijalo, au muulize mkufunzi wako.
Kazi ya Usomaji
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker