Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

244 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Kama kawaida unapaswa kuja na Fomu ya Ripoti ya Usomaji yenye muhtasari wako wa maeneo ya usomaji ya wiki. Pia, ni muhimu uwe umechagua maandiko kwa ajili ya Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (eksejesia), na ukabidhi mapendekezo yako kuhusiana na Kazi ya Huduma.

Kazi Zingine Ukurasa wa 126  6

Somo linalofuata, Mungu Roho Mtakatifu: Nafsi ya Roho Mtakatifu , linalenga juu ya Mungu Roho kama nafsi ya tatu ya Mungu mmoja wa Utatu. Tutazungumza kuhusu Roho kama “Mpaji wa Uhai” na kuonyesha jinsi majina, vyeo, na ishara za Roho katika Maandiko zinavyomwonyesha yeye kama chanzo na mtegemezaji wa maisha ya kimwili na ya kiroho na kama nafsi iliyo kazini ili kuvifanya vitu vyote kuwa vipya. Nafsi ya Roho Mtakatifu ni halisi na muhimu kama Mungu Baba na Mungu Mwana. Roho ametumwa na Baba na Mwana ulimwenguni ili tuweze kupata ushirika wa upendo pamoja nao na ili tuweze kutiwa nguvu kutii amri za Mungu na kutimiza utume wake. Ombi letu ni kwamba kiwango chenu cha kumtegemea Roho Mtakatifu kitakua mnapojifunza Maandiko pamoja. Tafadhali tazama nyenzo zifuatazo katika kitabu cha Theolojia katika Picha: Orodha ya A-Z ya Vielelezo, Chati, Michoro na Makala Muhimu za TUMI : • Ndani ya Kristo , ukurasa wa 373 • Masihi Yesu: Utimilifu wa Vivuli vya Agano la Kale , ukurasa wa 265 • Maadili ya Agano Jipya: Kuishi kwa kugeuka chini - Katika ufalme wa Mungu , ukurasa wa 208 • Unabii wa Kimasihi Uliotajwa katika Agano Jipya , ukurasa wa 472 • Kuhubiri na Kufundisha Yesu wa Nazareti kama Masihi na Bwana , ukurasa wa 131

Kuelekea Somo Linalofuata

KWA UTAFITI ZAIDI

3

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker