Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | MUNGU ROHO MTAKAT I FU : NAF S I YA ROHO MTAKAT I FU / 251

b. Kazi ya Roho Mtakatifu katika upaji [utunzaji]: Mpaji wa uzima. (1) Roho yupo kazini kuumba, kufanya upya na kutoa kwa ajili ya aina zote za uzima zilizopo katika uumbaji wake. (2) AK: Zab. 104:29-30; Isa. 32:14-15 (3) AJ: Yoh. 6:63; Rum. 8:2, 6, 11

Kotekote katika ulimwengu, nguvu kubwa sana zinazofanya kazi katika jua, nyota, na makundi ya nyota hutiwa nguvu na Roho wa Mungu. Nishati na nguvu zote zipo kwa uweza wa Roho Mtakatifu. ~ J. Rodman Williams

2. Ishara za Roho Mtakatifu katika Biblia zinamfunua yeye kama Mpaji wa uzima.

a. Maji – chanzo cha Uzima. (1) Isaya 44:2-4a (2) Yohana 7:37-39 (3) Yohana 4:14 (4) 1 Wakorintho 6:11 (linganisha na Tito 3:5) (5) Ufunuo 22:17

Tazama Ray Pritchard, Names of the Holy Spirit . Chicago: Moody Press, 1995. kurasa za 57, 69, 77, 100, 187.

b. Mafuta – utegemezaji wa maisha. Katika nyakati za kibiblia, mafuta ya zeituni

4

yalitumiwa kwa ajili ya chakula na dawa na vile vile kama nishati za taa ambazo ziliwashwa ili kutoa mwanga ndani ya nyumba. Mafuta hayo yalikuwa muhimu sana katika maisha ya kila siku kiasi kwamba yalikuwa ni ishara ya ustawi. Mtu asingeweza kufikiria mafuta bila kufikiria uponyaji, usalama na utele. Yalitegemeza maisha. Mafuta kama mfano wa Roho Mtakatifu, yalichukua jukumu muhimu zaidi kama ishara kwa sababu ya matumizi ya kibiblia ya upako [yaani kutia mafuta]. Manabii (1 Wafalme 19:16), Makuhani (Kut. 28:41), na Wafalme (2 Sam. 2:4; 1 Wafalme 1:34) walikuwa wakipakwa mafuta ili kuwatenga kwa ajili ya huduma. Kumiminwa huku kwa mafuta kulikuwa ni ishara ambayo ilionyesha waziwazi kwamba mtu huyo amempokea Roho Mtakatifu juu yake. Kutiwa mafuta kulionyesha kwamba Mungu alikuwa amemchagua na kumtayarisha mtu ili kuwahudumia watu wake afya,

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker