Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

250 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Mwanzo 1:2 - “pamoja na upepo wa kiungu ”

b. Kazi ya Roho katika uumbaji wa kimwili inafanana na kazi ya Roho katika “uumbaji mpya” (wokovu) (tazama, Yohana 3). Yohana 3:8 - Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.

2. Roho ni pumzi ya Mungu ambayo inawaleta wanadamu katika uzima.

a. Mwanadamu wa kwanza, Mwa. 2:7

b. Wanadamu wote, Ayu 33:4, 6

B. Roho anahusika kwa karibu katika kutegemeza uzima katika ulimwengu.

1. Fundisho la Upaji wa Kiungu.

4

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

a. Ufafanuzi: Neno “upaji” [katika mantiki ya utunzaji, providence ] linatokana na neno kutoa . Kwa njia ya upaji wake Mungu anategemeza, anatawala, na kulinda uzima alioutoa katika dunia na kuuongoza hadi kwenye hatima ambayo kwa ajili yake uliumbwa.

Maana ya msingi ya upaji [utunzaji] ni kuona mbele, au kutoa. Suala la upaji [utunzaji] linahusu jinsi Mungu anavyofikiria mbele zaidi katika kutunza viumbe vyote. . . . Upaji wa Mungu hutazama mbele na kubaini mahitaji ambayo bado hayajatambuliwa na viumbe. Lakini zaidi ya kuona mbele tu, upaji unahusiana na uhifadhi wa kila siku wa Mungu kwa ulimwengu katika hatari zake.

~ Thomas C. Oden. The Living God . uk. 271.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker