Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 4 | MUNGU ROHO MTAKAT I FU : NAF S I YA ROHO MTAKAT I FU / 255
Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kupitia maudhui ya vieo. Yanalenga utambulisho wa Roho kama mpaji wa uzima. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi iwezekanavyo, na tumia Maandiko kujenga hoja zako. 1. Elezea namna ambavyo mawazo ya Agano la Kale na ya Agano Jipya kuhusu Roho wa Mungu yanafanana, na namna ambavyo yanatofautiana. 2. Jukumu la Roho katika uumbaji ni lipi? Hili linaonyesha nini kuhusiana na jukumu lake katika wokovu wa waamini (uumbaji mpya)? 3. Upaji [utunzaji] ni nini? Je, Roho ana sehemu gani katika utunzaji wa Mungu kwa ulimwengu? 4. Je, ni ishara gani kuu za Roho Mtakatifu katika Maandiko? Je, haya yanachangiaje katika ufahamu wetu wa Roho kama ndiye atoaye uzima? 5. Je, ni vyeo gani vya kibiblia vya Roho Mtakatifu ambavyo vinasisitiza huduma yake ya kutoa uzima? 6. Ni kwa namna gani huduma ya Roho huleta tumaini kwa waamini wote? Somo hili linahusu Nafsi ya Roho Mtakatifu. Katika mada hii tumejadili kweli zifuatazo: • Maandiko yanamfunua Mungu Roho Mtakatifu kama Mpaji wa Uzima ambaye ni muumbaji na mtegemezaji wa maisha yote. • Picha na ishara zinazotumiwa kumwelezea Roho Mtakatifu katika Biblia zinasisitiza ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni Mpaji na Mtegemezaji wa uhai wote. • Majina ya kimaandiko ya Roho Mtakatifu yanaonyesha upeo wa huduma yake ya kutoa uzima na hata kumtaja moja kwa moja kama “Roho wa Uzima.” • Kusudi la utoaji uzima la Roho Mtakatifu linamaanisha kwamba yeye ndiye chanzo cha tumaini kwa watu binafsi, kwa Kanisa na kwa ulimwengu.
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
UHUSIANISHAJI
Muhtasari wa Dhana Muhimu Ukurasa wa 133 11
4
T H E O L O J I A N A M A A D I L I
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker