Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

256 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Sasa ni wakati wako wa kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu mambo ambayo tumejifunza katika somo hili la “Nafsi ya Roho Mtakatifu.” Hata theolojia ya kinadharia zaidi haikusudiwi kuwa “zoezi la kielimu” tu. Kweli za kitheolojia zinakusudiwa kuathiri maisha yetu. Sehemu muhimu zaidi ya kipengele hiki cha maswali na majibu kuhusu Roho Mtakatifu, ni kugundua jinsi Mungu anavyotaka kutubadilisha kupitia yale tuliyojifunza. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia yale ambayo umejifunza hivi punde? Pengine baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na ya msingi zaidi. • Mojawapo ya tabia zinazofanana za “imani potofu” na ambazo zimekuwepo nyakati zote ni kwamba wanafundisha mafundisho yasiyo sahihi kuhusu Mungu. (Iwapo mtu anafundisha upotofu juu ya asili ya Mungu na kweli yake tofauti na jinsi inavyofunuliwa katika Maandiko, hakuna namna anavyoweza kuwakilisha vyema kazi ya Mungu ulimwenguni). Je, ni makosa ya aina gani yanayoweza kutokea kutokana na kufikiria vibaya kuhusu nafsi ya Roho Mtakatifu? • Ufahamu wa ukweli kwamba Roho Mtakatifu ametumwa kama Msaidizi ( paracletos ), aliyeitwa kuwa pamoja nasi na kuwakilisha uwepo ulio hai wa Yesu katikati yetu, unamatokeo gani kwa mwamini? • Je, maelezo kuhusu Roho Mtakatifu kama “kifungo cha upendo” kati ya Baba na Mwana yanaathirije uelewa wetu wa jukumu la Roho katika maisha yetu binafsi na makusanyiko ya Kanisa? • Taja baadhi ya njia zinazofaa ambazo makanisa yetu yanaweza “kumwabudu na kumtukuza Roho” pamoja na Baba na Mwana. • Je, kuna umuhimu wowote katika ukweli kwamba maneno yanayotumika kutafsiri neno “Roho” katika Kiebrania na Kiyunani pia yanamaanisha “pumzi” au “upepo”? Je, dhana hizi zinazohusiana kwa karibu zinatuambia nini kuhusu kazi ya Roho? • Roho Mtakatifu ametendaje kazi kama Mpaji wa Uzima katika maisha yako binafsi? Je, uwezo wake wa kutoa uzima umeleta utofauti gani katika mtazamo wetu juu ya huduma? • Kati ya ishara za kimaandiko zinazomwakilisha Roho Mtakatifu, ni zipi zimekuwa muhimu zaidi katika maisha yako binafsi? Je, zimekusaidiaje kumwelewa Roho Mtakatifu? Na zimeathiri vipi uelewa wako wa uongozi wa Kikristo?

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi Ukurasa wa 133  12

4

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker