Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | MUNGU ROHO MTAKAT I FU : NAF S I YA ROHO MTAKAT I FU / 257

• Kama Wakristo ambao Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu, mara nyingi tunafikiria kazi ya Roho katika mtazamo wa kibinafsi sana: Roho anaishi ndani yangu na kunisaidia kumjua na kumtii Mungu. Je, ni jambo la kawaida kwako pia kumfikiria Roho Mtakatifu kama mwenye kuutegemeza uumbaji wote na ambaye anautayarisha ulimwengu kwa ajili ya utawala ujao wa Kristo? (Elezea jibu lako).

MIFANOHALISI

Kuwa Tayari Kutoa Jibu Unafundisha somo la Roho Mtakatifu katika darasa la Biblia ndani ya kanisa lako na unawakumbusha wanafunzi wako kwamba ni halali kabisa Yeye kuitwa Bwana na Mpaji wa Uzima. Mgeni aitwae Sue, ambaye amekuja kwenye mafundisho mara chache tu, anafurahia anaposikia maelezo yako. Sue anasema, “Kwa kawaida mimi hushiriki ibada katika Kanisa la Unity mtaa wa chini hapo na walinipa kitabu kinachozungumzia jambo hilo hilo.” Anachomoa kitabu na kutafuta kurasa zenye nukuu hizi, “Mungu ni Roho, au kani ya uumbaji ambayo ndiyo chanzo cha vitu vyote vinavyoonekana. . . . Mungu sio kiumbe au nafsi yenye uzima, utashi, upendo na nguvu. . . . Mungu ni yule asiyeonekana, asiyeshikika, lakini ni halisi sana, ni kitu tunachoita uzima. . . . Kila mwamba, mti, mnyama, kila kitu kinachoonekana, ni udhihirisho wa Roho mmoja – Mungu – tofauti ni kiwango tu cha udhihirisho; na kila moja ya njia hizo zisizo na idadi za udhihirisho, au upekee wa kila kimoja, japokuwa si muhimu sana, lakini bado inamjumuisha yeye mzima” ( Lessons In Truth, H. Emilie Cady , kilichochapishwa na The Unity School of Christianity, kurasa za 18, 19-20). Mara moja unatambua kwamba amekuwa akijifunza na kikundi ambacho hakina fundisho sahihi la Mungu au Utatu. Utamwambia nini Sue, na hicho kikundi cha mafunzo ya Biblia, unapozijibu nukuu alizozisoma? Kutafuta Usahihi Carlos ni mwamini mpya katika Kristo ambaye anajaribu kuelewa kile ambacho Biblia inafundisha kuhusu Roho Mtakatifu. Anasema, “Ni rahisi kwangu kuelewa Yesu ni nani. Ninaweza kusoma hadithi kumhusu katika Maandiko na kujua yale hasa aliyosema na kufanya. Nilipoweka tumaini langu katika Kristo kwa ajili ya wokovu, nilihisi kama Petro alivyohisi alipomwambia Bwana kwamba hangeweza kwenda popote pengine kwa sababu Yesu alikuwa na “maneno ya uzima wa milele.” Lakini Roho Mtakatifu anaonekana kuwa fumbo kubwa sana. Siwezi kufikiria jinsi alivyo na sina uhakika ni jinsi gani ninapaswa kuwa na uhusiano naye. Unaweza kunisaidia kujua?”

1

Ukurasa wa 133  13

4

T H E O L O J I A N A M A A D I L I

2

Ukurasa wa 134  14

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker